Haya ndio madarasa mapya ya shule ya msingi kipito ambapo kuanzia darasa la kwanza hadi la saba wanasomea katika vyumba viwili vya madarasa haya
hivi ni vyoo vya shule na walimu wa shule ya msingi Kibito
hivi ni vyoo vya shule na walimu wa shule ya msingi Kibito
shule ya msingi Kibito
wanafunzi wakipeana zamu za kusomea madarasa hayo yenye vumbi
mwalimu Mlelwa mmoja wa walimu wa shule hiyo
mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kibito Mwalimu Nikodem Haule shule,shule hiyo ina walimu watatu
Shule hiyo
ambayo awali ilianzishawa na mwananchi mmoja anayejulikana kwa jina la Aulelian
Ngailo Wipata kwa kujenga vyumba viwili vya madarasa kwa kutumia ujenzi wa
mianzi na udongo na juu ikiezekwa nyasi
imeendelea kuwa katika mazingira magumu hali iliyo mlazimu mwananchi huyo
kujitolea tena kujenga chumba kimoja cha
darasa na ofisi kwa kutumia tofari za kuchona na kuwaacha wananchi wa eneo hilo
wakichangia nguvu katika ujenzi wa darasa moja.
Akiongea na
mwandishi wa habari hii Bw.Ngailo alisema kuwa kutoendelea kwa shule hiyo mpaka
sasa na kusababisha wanafunzi wa madarasa yote kusomea vyumba viwili vya
madarasa imesababishwa na uzembe wa Mwenyekiti wa kitongoji ambaye amekuwa
nyuma katika kuhamasisha wananchi kufanya kazi ya kimaendeleo katika ujenzi wa
shule hiyo.
Bw.Ngailo
alisema kuwa awali shule hiyo ilianza kwa kasi katika ujenzi hali iliyopelekea
yeye kujitolea kujenga chumba kimoja cha darasa na ofisi ya walimu lakini baada
ya kuondoka uongozi uliokuwepo na kuingia uongopzi mpya hali imezidi kuwa mbaya
kwani hakuna kinachoendelea shuleni hapo na kuwaacha wanafunzi wakisomea
mazingira mabaya ambayo ni aibu kwa wilaya ya Ludewa.
“uongozi
ulioingia wa vijana hakuna hata mzee mmoja katika kamati ya ushauli,wanaamua
wanavyoona wenyewe kwani Serikali ilileta saruji mifuko miambili lakini hata
vyumba hivyo viwili vya madarasa havijasakafiwa na saruji iko stoo tu
ikiendelea kuharibika na inamuda wa miaka miwili mpaka sasa,sisi wazee tumeona
tuwaache wafanye wawezalo maana tukiwauliza wanadai tunawaingilia”,alisema
Bw.Ngailo.
Akijibu
tuhuma hizo za wazee Mwenyekiti wa kitongozi cha Kibito ambaye pia ndiye
msimamizi wa kazi za kimaendeleo shuleni hapo Bw.Andrea Mgimba alisema kuwa
yeye na kamati yake wamejitahidi katika ujenzi wa shule hiyo mpaka hapo
ilipofikia nakini yeye siye kikwazo cha maendeleo katika ujenzi wa shule hiyo.
Bw.Mgimba
alielekeza lawama Serikalini kuwa imeizira shule hiyo licha ya kuleta mifuko
200 ya saruji na kushindwa kufanyiwa kazi kwa muda wa miaka miwili hivi sasa
kwani alisema kuwa kitongoji hicho kila wakazi wachache hali inayosababisha
washindwe kufikia malengo katika ujenzi wa vyumba vingine vya madarasa.
Aidha
mwalimu mkuu wa shule hiyo Mwalimu Nikodem Haule alikili kuwapo na changamoto
nyingi shuleni hapo ikiwepo upungufu wa vyumba vya madarasa na ukosefu wa vyoo vya
kisasa kwa matumizi ya walimu na wanafunzi hali ambayo ni hatari kwa afya kwani
inaweza kusababisha magonjwa ya mripuko muda wowote.
Mwalimu
Haule alisema kuwa shule hiyo imekuwa ikisaidiwa kwa kiasi kikubwa na diwani wa
kata hiyo mh.Mseya ambaye ameahidi kujenga vyumba vingine vya madarasa ili
kuwanusuru wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo ya msingi kipito.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment