Deo Ngalawa akipokelewa kwa maandamano Ludewa mjini
Deo Ngalawa akisalimiana na katibu tawala wa wilaya ya Ludewa Bw.Ulaya
Ngalawa akiwa katika Maandamano
maandamano yakiendelea kuelekea ofisi za ccm Ludewa mjini
Deo Ngalawa akiwa katika ofisi za ccm wilaya ya Ludewa
Mgombea
ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi(ccm)Deo Ngalawa jimbo la Ludewa ambaye
ni mrithi wa hayati Deo Filikunjombe amepokelewa kwa maandamano makubwa ya
kumuunga mkono na wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa wilayani hapo wakati
akitokea jijini Dar es Salaam.
Mapokezi
hayo makubwa yamekuja baada ya mwenyekiti
wa kamati kuu ya CCM rais mstaafu Dr.Jakaya Mrisho Kikwete kumpitisha rasmi
Bw.Ngalawa kuwa mgombea wa nafasi ya ubunge kwa jimbo ambapo katika kura za
maoni Bw.Ngalawa aliibuka mshindi dhidi ya wapinani wake tisa ambao alichuana
nao vikali kuisaka nafasi hiyo.
Licha ya
kuwa mgombea huyo anatoka chama cha mapinduzi lakini ameungwa mkono na vyama
vingine vya siasa kutokana na hali halisi kuwa Bw.Ngalawa hakuwahi kuwa na kashfa
yoyote wa kundi hivyo amekuwa ni mfano katika jamii ya Ludewa na anauwezo wa
kufuata nyayo za hayati Filikunjombe kimaendeleo kwani alishaitendea makubwa
wilaya ya Ludewa kwa kushirikiana na aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ludewa.
Akiongea
katika maandamano hayo jana yaliyoanzia shule ya Sekondari Chief Kidulile na
kumalizikia ofisi za ccm wilaya Bw.Titus Haule ambaye ni mwanachama wa chama cha Demokrasia na maendeleo
(CHADEMA) alisema kuwa wameamua kumuunga mkono Ngalawa kutokana na ukweli
kwamba hana ubaguzi pia amefanya makubwa ndani na nje ya Ludewa kimaendeleo.
Bw.Haule
alisema kuwa kamati kuu ya ccm imetumia busara kulipitisha jina la Ngalawa kwani
amekuwa ni msaada mkubwa katika jamii bila kubagua itikadi za vyama au dini
mfano mzuri ni ujenzi wa chuo cha ualimu kata ya Lupingu ambapo mpaka sasa
majengo yamesha kamilika bado ufunguzi pia ujenzi wa chuo cha Afya Ludewa Mjini
ambapo ujenzi unaendelea vizuri na hivyo vyote ni pesa yake mfukoni.
Alisema
richa ya ujenzi wa vyuo hivyo kwa pesa yake kama mwanaludewa pia ametoa misaada
ya mashine za ukamuaji wa mafuta ya Alizeti pia aliweza kununua magari ya
usafiri wa abilia na kuyapeleka maeneo magumu ambaye wananchi wa vijiji hivyo
walikuwa wakitembea kwa miguu kwa zaidi ya kilomita 35 kufuata huduma za kijamii makao makuu ya wilaya.
“Sisi
hatujali itikadi za vyama katika wilaya yetu tunachokiangalia ni mtu mpenda
maendeleo hivyo tunamuunga mkono kwa asilimia zote Ndalawa kama tulivyo muunga
mkono hayati Filikunjombe kutokana na ukweli usiopingika kuwa wote ni majembe
katika maenendeleo pia wenzetu wa ukawa baadhi yao walisherekea kifo cha
Filikunjombe jambo ambalo limewakera wanaludewa hali inayopelekea kila tukipita
mitaani tuonekane wabaya”,alisema Bw.Haule.
Bw.Haule
aliwataka wanaludewa kumuunga mkono Bw.Ngalawa ili kuweza kukamilisha mambo
mbalimbali ya kimaendeleo ambayo yaliachwa na hayati kwani hakuna mtu mwingine
wa kuyaendelea hayo zaidi ya Ngalawa ambaye tokea awali amekuwa akionesha
kuleta maendeleo Ludewa.
Aidha Deo
Ngalawa ambaye ndiye jina lake limepitishwa na kamati kuu ya ccm kuwa mgombea
wa ubunge jimbo la Ludewa alisema kuwa mchakato ndani ya chama ulikwisha hivyo
kilichobaki ni kuyavunja makundi na kuwa kitu kimoja katika suala zima la
maendeleo wilayani Ludewa.
Bw.Ngalawa
alisema kuwa atakamilisha mipango ya hayati Filikunjombe na kumuenzi kwa kuleta
maendeleo ya haraka hivyi hata waangusha wanaludewa katika maendeleo jambo la
msingi ni ushirikiano mzuri ambao utaleta nguvu ya pamoja kwani yeye peke yake
hawezi kufanikisha maendeleo hivyo aliwaomba wananchi kuungana bila kujali
itikadi za vyama na dini wala kabila.
Naye katibu
wa ccm Ludewa Bw.Rusiano Mbosa aliwataka wananchi kuhakikisha Bw.Ngalawa
anapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi unaotarajia kufanyika hivi karibuni
kwani kwa kufanya hizo wanaludewa watakuwa wamemuenzi hayati Deo Filikunjombe
ambaye alikuwa mpiganaji ndani ya chama chake cha CCM.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment