Mgimba ameshachukua fomu ya ubunge ndani ya ccm jimbo la Ludewa anasubiri ridhaa ya wajumbe
Mhandisi Zefania Chaula ameshachukua fomu ya ubunge ndani ya ccm jimbo la Ludewa anasubiri ridhaa ya wajumbe
Simon Ngatunga ameshachukua fomu ya ubunge ndani ya ccm jimbo la Ludewa anasubiri ridhaa ya wajumbe
Mgaya ameshachukua fomu ya ubunge ndani ya ccm jimbo la Ludewa anasubiri ridhaa ya wajumbe
Phd Mtitu na Masanja wameshachukua fomu ya ubunge ndani ya ccm jimbo la Ludewa wanasubiri ridhaa ya wajumbe
Mtitu ameshachukua fomu ya ubunge ndani ya ccm jimbo la Ludewa anasubiri ridhaa ya wajumbe
Philipo Filikunjombe ameshachukua fomu ya ubunge ndani ya ccm jimbo la Ludewa anasubiri ridhaa ya wajumbe
Philipo Filikunjombe ameshachukua fomu ya ubunge ndani ya ccm jimbo la Ludewa anasubiri ridhaa ya wajumbe
Emmanuel Mgaya (Masanja)mwenye suti nyeusi akiwa na Nickson Mahundi mmiriki wa mtandao huu ameshachukua fomu ya ubunge ndani ya ccm jimbo la Ludewa anasubiri ridhaa ya wajumbe
Mchuano
mkali wa wagombea nafasi ya ubunge umeibuka katika jimbo la Ludewa ambapo mpaka
sasa ni zaidi ya watangaza nia tisa wameshachukua fomu ya kuwania nafasi hiyo
iliyoachwa wazi na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Ludewa hayati Deo
Filikunjombe alifariki kwa ajali ya chopa akitokea jijini Dar es salaam kwenda
jimboni kwake kwaajili ya kufunga kampeni.
Akiongea na
waandishi wa habari katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Ludewa Bw.Lusiano
Mbosa alisema kuwa mpaka siku ya leo tayari wagombea waliochukua fomu katika
ofisi yake wameshafikia tisa na wengine wako njiani wakiahidi kuchukua ili kuingia
katika kinyang’anyilo hicho ambapo kula mmoja akiwa na matumaini ya kuchukua
ushindi na kukiwakirisha chama chake.
Bw.Mbosa
alisema kuwa jambo la msingi kwa wagombea ni moja tu la kusubiri mchakato wa
kura za maoni ufanyike ili kumpata mmoja ambaye atapeperusha bendera ya chama
hivyo kwa wale ambao hawajiamini kutokana na baadhi ya wagombea kuwa na majina
makubwa isiwape taabu sana maana wenye maamuzi makubwa ni wajumbe ambao ni
wapiga kura.
Aidha mpaka
sasa baadhi ya waliochukua fomu ni Deo
Ngalawa,Philipo Filikunjombe,Emmanuel Mgaya Masanja,Simon Ngatunga na wengine
ambao wako katika harakati hizo lakini mpaka sasa bado haijajulikana ni nani
ataweza kuvivaa viatu vya hayati Deo Filikunjombe.
Tunawakaribisha
wote na mwanachama yeyote anaruhusiwa kuchukua fomu kwa mujibu wa katiba ya ccm
kwani kura za wajumbe ndizo zitakazo amua yupi atafaa kuchukua nafasi hiyo
hivyo tunasubiri ratiba ya upigaji kura za maoni kutoka makao makuu na
tukishapata ratiba tutaitangaza tarehe ya kura ya maoni.
Naye
Bw.Emmanuel Mgaya alimaarufu kwa jina la Masanja Mkandamizaji ambaye ni
muigizaji wa Ze Original Comedy ambaye amechukua fomu siku ya jana kwa mbwembwe
kubwa alionesha kuwatisha wapinzani wake kutokana na jina lake lilivyo kubwa
wilayani hapa na Tanzania kwa ujumla hivyo kuwafanya wakazi wa Ludewa Mjini
kumfuata na kumpa moyo juu ya kinyanga’nyilo hicho.
Bw.Mgaya
alisema kuwa anania ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa wilaya ya Ludewa
kutokana na ukweli kwamba yeye ni mzaliwa wa wilaya hii hivyo anazifahamu shida
na matatizo ya wananchi wa wilaya ya Ludewa kupita mgombea yeyote ambaye
amechukua fomu ya nafasi hiyo.
Alisema kuwa
richa ya kuwa kumekuwa na wagombea wengi wanaoitaka nafasi hiyo yeye ndiye mtu
pekee ambaye ataweza kuvivaa viatu vya hayati Deo Filikunjombe katika utendaji
wa kazi hata hivyo alikiri kuwa wajumbe ndio wenye maamuzi ya mwisho hivyo
akinda au akishindwa atamuunga mkono yeyote atakayepitishwa na chama cha
mapinduzi kwa kuwa yeye kama mwanaludewa anapaswa kuungana na wanaludewa
wengine katika kuleta maendeleo kwa wananchi.
Baadhi ya
wananchi wamekuwa na maoni tofauti katika mtifuano huo kutokana na ukweli ambao
haupingiki kuwa hakuna kma Deo Filikunjombe hivyo wanachohitaji ni kumpata mtu
ambaye kwa kiasi furani ataweza kuyafanya japo kidogo mambo yaliyowanywa na
mpendwa mbunge wao enzi za uhai wake
hali iliyofanya akubarike na kila rika.
Mmoja wa
wananchi hao Bw.Amoniche Mtweve alisema kuwa mpaka sasa ni majina matatu ndiyo
yanayotamba vinywani mwa wananchi wa kurithi nafasi hiyo ambao ni Deo Ngalawa
ambaye amekuwa na jina kubwa pia yupo mdogo wa hayati Filikunjombe ambaye ni
Philipo Filikunjombe naye pia anatajwa na wananchi na wamwisho ni Emmanuel
Mgaya Masanja ambaye amekuja kwa kasi na kubadiri upepo wa kisiasa kwa wengine.
Alipotakiwa
kutoa sababu kwanini majina haya yanatajwa sana Bw.Mtweve alisema Kuwa Deo
Ngalawa amekuwa akishirikiana katika maendeleo na wananchi tokea muda mrefu
hivyo wananchi wanamuona ni mwenzao katika maendeleo,Philipo Filikunjombe
wananchi wanahisi anajua mipango ya marehemu kaka yake hivyo anaweza
kuiendeleza akipewa nafasi na Emmanuel Mgaya Masanja anabebwa na umaarufu
aliokuwa nao nchii hivyo naye bado ananafasi ya kuwa kiongozi bora.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment