Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

May 12, 2015

WANANCHI WA WILAYA YA LUDEWA WANAOISHI MBALI WENYE MAENEO NCHUNCHUMC NA LIGANGA WATAKIWA KURUDI ILI WAWEZE KUTHAMINISHA MAENEO YAO.

  Ofisa Ardhi mshauli wa wilaya ya Ludewa Bw.Joseph Kamonga



Wananchi wa wilaya ya Ludewa wanaoishi mbali na wilaya hiyo wenye maeneo katika migodi ya chuma liganga na makaa ya mawe Nchuchuma wametakiwa kurudi katika maeneo yao ili kushiriki katika zoezi la uthaminishaji ili waweze kulipwa fidia zao pasipo mgogoro.

Hayo yamesemwa leo na ofisa ardhi mshauri wa wilaya ya Ludewa Bw.Joseph Kamonga wakati akihojiwa na waandishi wa habari kuhusiana na watu wenye maeneo katika maeneo ya migodi hiyo lakini wanaishi mikoa mingine na wilaya nyingine tofauti na wilaya ya Ludewa.

Bw.Kamonga alisema kuwa ni vema wenye maeneo yao ambao hawaishi wilaya ya Ludewa wangerudi mara moja ili waweze kushiriki ipasavyo kani baada ya kukamilisha uthaminishaji hawataweza kurudia zoezi hilo tena.

No comments: