mtambo ukiwa kazini
Filikunjombe akikagua barabara mpya ya Mawengi Makonde
Filikunjombe akiwa amechoka kutembea kutoka kata ya Mawengi kuelekea kata ya Makonde,nyuma yake ni katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM mkoa wa Njombe Bw.Onoratus Mgaya
Hii ndiyi barabra inayotoka kata ya Mawengi kuelekea kata ya Makonde
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Bw.Willium Waziri akiongea na wananchi
Filikunjombe akiongea na wananchi wa kata za Makonde,Lifuma na Mawengi mara baada ya uzinduzi
Ujenzi wa
barabara ya kijiji cha Mawengi kwenda kata za Makonde na Lifuma mwambao wa ziwa Nyasa wilayani Ludewa katika
mkoa wa Njombe kwa kiwango cha changalawe umezinduliwa rasmi jana na mbunge wa
jimbo la Ludewa Mh.Deo Filikunjombe
Akizindua
ujenzi wa barabara hiyo inayofadhiriwa na ubalozi wa Japani Filikunjombe
alisema kwa miaka mingi wananchi wa kata za mwambao wa ziwa Nyasa wamekuwa wakitumia
usafiri wa majini katika shughuri zao mbalimbali lakini Serikali ya chama cha
mapinduzi imekisikia kilio cha watu wa mwambao hivyo imeona ni bora kutoboa
barabara inayofuka katika kata hizo ili kurahisisha maisha ya wananchi.
Filikunjombe
alisema kuwa wananchi wa mwambao wa ziwa nyasa wamekuwa wakipata mahitaji yao
kupitia wilaya jirani ya Kyela kutokana na kutokuwa na barabra ya gari
inayoweza kuwafikisha katika makao makuu ya wilaya yao hivyo ujenzi wa barabara
hiyo ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa kata za Makonde na Lifuma.
Hata hivyo
aliwataka wakandarasi wa mradi huo wa barabara kuwa waaminifu na kufanya kazi
kwa umakini mkubwa kwani kumekuwa na tabia ya baadhi ya wananchi na wakandarasi
kutokuwa waaminifu kwa kuiba vipuli na mafuta ya mitambo hali ambayo inarudisha
maendeleo nyuma.
Filikunjombe
alisema imekuwa ni tabia mbaya inayoendelea kuzoeleka nchini ya wizi wa mafuta
wakati Serikali imepanga bajeti ya kutosha katika matengenezo ya barabara
mbalimbali lakini baadhi ya watu hutumia miradi hiyo kujinufaisha kwa kuiba
vipuli na mafuta hivyo atakayebainika katika ujenzi wa barabara zote wilayani
Ludewa Sheria itachukua mkoando wake.
“Leo
tunazindua ujenzi wa barabara ya Mawengi kwenda Makonde ni barabara ambayo inaumuhimu
mkubwa kwa wananchi wa mwambao lakini wako watu wanafikiria kuiba mafuta ya
mitambo na vipuli,nawaomba tabia hiyo ikome mara moja kwani serikali imeona
ilifanye hili ili kuwaletea maendeleo wananchi wa maeneo haya hivyo nalioamna
jeshi la polisi yeyote atakayebainika akamatwe na afikishwe mbele ya sheria
lakini nawaomba wananchi kuwa walinzi wa miradi yenu ili ikamilike haraka”,alisema
Filikunjombe.
Barabara
hiyo ambayo itaziunganisha kata tatu na vijiji vingi vya mwambao wa Ziwa Nyasa
inakuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa maeneo hayo kutokana na wananchi wengi kuwa
na shauku ya kufanya biashara ya samaki kwa kiasi kikubwa tofauti na awali
walikuwa wakibeba samaki kwa kichwa na kutembea umbali kwa kilomita 34 hadi
mawengi kwaajili ya kuziuza na kujipatia kipato.
Aidha
Bw.Erasto Magombola mkazi wa kijiji cha mawengi alisifu Serikali kwa kuiangalia
barabara hiyo kutokana na wananchi wa maeneo ya mwambao kusafirisha wagonjwa
hadi kijiji cha mawengi kwa kuwabeba katika mchela hivyo barabara hiyo ni ukombozi
mkubwa kwao.
Bw.Magombola
alisema kuwa kutokana na ujenzi wa barabara baadhi ya wafanya biashara wa
sanmaki na maharage watapata fulsa ya kufanya biashara hiyo kwa urahisi kwani
samaki wa ziwa Nyasa wamekuwa wakiuzwa zaidi wilaya ya Kyela wakati wavuvi wako
wilaya ya Ludewa haya yote yalisababishwa na ubovu wa barabara.
Kuhusu wizi
wa mafuta Bw.Mgombola alisema kuwa yeye kama mwananchi na muhasibu wa kijiji
cha Mawengi atashirikiana na uongozi wa kijiji na kata kuwazibiti wezi hapo na
hawatawafumbia macho mafanyakazi wa mradi huo ambao watakwenda kinyume na
maadili ya kazi zao.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment