Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

May 15, 2015

LUANA WAAHIDIWA KUJENGEWA BARABARA KUTOKA STAND HADI KANISA KATOLIKI,UMEME WAENDELEA KUSAMBAZWA MITAANI

Filikunjombe akiwa na wafanyakazi wa shirika la Tanesco wilayani Ludewa katika kijij cha Luana wakishusha Trasfoma



 Filikunjombe akisaidia kushusha waya wa kusambazia umeme katika vitongoji vya kijiji cha Luana




Filikunjombe akiongea na wananchi wa kijiji cha Luana wilayani Ludewa

Mbunge wa jimbo la Ludewa katika mkoa wa Njombe Mh.Deo Filikunjombe amewaahidi wananchi wa kijiji cha Luana kuwa anatafuta fedha za kuikarabati barabara ya kutoka stand ya Luana hadi kanisa Katoriki kutokana na barabara hiyo kutopitika msimu wa mvua.


Akihutubia katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Luana Filikunjombe alisema kuwa imekuwa ni vigumu sana wakati wa mvua gari kupita katika barabara hiyo hivyo anatafua fedha ili aweze kuikarabati haraka iwezekanavyo ili iweze kupitika misimu yote ya mwaka .


Alisema licha ya ukarabati wa barabara hiyo pia usambazaji wa umeme katika vitongozi vya Luana utakamilika ndani ya mwezi mmoja ili uharakisha maendeleo katika kijiji hicho.

No comments: