Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

November 28, 2014

WALIMU NA WANAFUNZI WAFYATUA TOFARI ZA NYUMBA YA MWALIMU BAADA YA WANANCHI KUSUSIA.

moja ya matanuru ya tofari ambazo zimefyatuliwa na wanafunzi pamoja na walimu zikiwa zimeshachomwa tayari kwa kuanza ujenzi
madarasa ambayo yameshakarabatiwa


madarasa yasiyo karabatiwa
Mwalimu mkuu wa shule ya sekodari ya makonde Oraphy Mwinuka akitoa ufafanuzi juu ya mgomo wa wananchi
Katibu wa Mbunge Filikunjombe Bw.Stanley Gowele akiongea na wananchi wa kijiji cha Makonde
Nyumba ya Mwalimu ambayo imekarabatiwa na wanafunzi kwa kushirikiana na walimu
Madarasa yasiyokarabatiwa
kikao na mkuu wa shule kikiendelea




Walimu na wanafunzi wa shule ya Sekondari Makonde wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wameanza ufyatuaji wa matofari ili kuweza kujenga nyumba ya mwalimu wa kike kutokana na wananchi wa kata nne zinazomiliki shule hiyo kususia kufanya maendeleo ya ujenzi.


Akizungumza katika ziara ya katibu wa mbunge wa jimbo la Ludewa mkuu wa shule hiyo mwalimu Oraphy Mwinuka alisema kutokana na uhaba wa nyumba za walimu imebidi kuunganisha nguvu za walimu na wanafunzi kufyatua matofari yatakayoweza kufanya ujenzi huo.


Mwalimu Mwinuka alisema shule hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo uhaba wa nyumba za walimu hali inayosababisha kutokuwa na mwalimu wa kike kutokana na kukosa mahala pakuishi hivyo hakuna namna ni lazima nyumba moja ijengwe ili apatikane mwalimu wa kike.


Alisema shule ya sekondari Makonde ni shule ya kata  ambayo iko kata ya Makonde mwambao mwa ziwa Nyasa lakini wenye dhamana ya kuijenga shule hiyo ni kata nne ambazo ni kata ya Makonde,Lifuma,Kilondo na kata ya Lumbila lakini mpaka sasa kata hizo hazijihusishi na ujenzi wa shule hiyo licha ya kuwa ni ukombozi mkubwa wa kielimu kwa kata za mwambao.


“tumeshafyatua tofari elfu kumi na tayari tumezichoma,pia tunamalizia ukarabati wa nyumba moja ili walimu waanze kuhamia hata kama ni nyumba moja ninaimani watakaa walimu vijana watano hatuna namna kutokana na wananchi wa maeneo haya kuwa wakaidi upande wa elimu licha ya kuwa tumepeleka malalamiko ngazi zote lakini hakuna majibu”,alisema mwalimu Mwinuka.


Kuhusu wanafunzi wakike kugoma kuishi hostel mwalimu Mwinuka alisema kumekumwa na uvumi unaotolewa na vijana wa kiume ambao si wanafunzi kutokana na tama zao za kimwili kuwa shule hiyo inahitaji wanafunzi wawili wa kuzindikia hivyo kama watathubutu kuishi katika hostel ni lazima wanafunzi wawili watapoteza maisha.


Alisema mpaka sasa ni idadi ya wanafunzi wachache ndio wanaoishi hostel na hakuna kilichotokea mpaka sasa hivyo uvumi huo wa baadhi ya vijana ni uongo hivyo wazazi wanatakiwa kuwalazimisha watoto wao kuishi hostel ili kupunguza uwezekano wa upatikanaji wa ujauzito kwa wanafunzi wa kike.


Ofisa mtendaji kata wa kata ya Makonde Bw.Augan Mhagama alikiri kuwepo kwa matatizo katika shule hiyo hasa wananchi wa kata yake na kata jirani ya Lifuma kususia kufanya maendeleo ya ujenzi wa nyumba za walimu kutokana na kata za Kilondo na Lumbila kutoshiriki ujenzi wa shule hiyo licha ya kuwa wanafunzi kutoka kata hizo wanasoma shuleni hapo.


Bw.Mhagama alisema chanzo cha migogoro ya ujenzi wa shule hiyo ni viongozi wa kata hizo kutokuwa na ushirikiano licha ya kuwa mara kwa mara wamekuwa wakindikiwa barua na mkuu wa shule katika mikutano ya pamoja ili kuhakikisha maendeleo yanapatikana lakini wamekuwa wakikaidi wito huo.


Aidha katibu wa mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe Bw.Stanley Gowele alimuagiza katibu tarafa wa tarafa ya mwambao kuwaita watendaji wa kata zote nne pamoja na madiwani wa kata hizo kukaa pamoja na kuona namna ya kufanya ili kuinusuru shule hiyo.


Bw.Gowele alisema hakuna haja ya kulumbana na viongozi wa kata hizo bali ni kukaa pamoja na kuona namna ya kufanya kwani elimu ni ukombozi mkubwa kwa vijana hivyo anayebisha kufanya maendeleo kwaajili ya shule hivyo achukuliwe hatua za kisheria.


Mwisho.














No comments: