MKUU WA MKOA IRINGA AKABIDHI MABATI 371 KWA HALMASHAURI
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa ametoa mchango wa mabati 371 kwa halmashauri za
wilaya ya Iringa kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa maabara kwa baadhi ya
shule za serikali za kata.
Mchango
huo ulikabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Juma Masenza kwa Mkuu
wa Wilaya ya Iringa, Leticia Warioba katika hafla fupi ya makabidhiano
iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa leo.
Wilaya ya Iringa ina halmashauri mbili ambazo ni Halmashauriya Manispaa ya Iringa na halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Masenza
alisema kuwa mchango huo ni kwa ajili ya kuunga juhudi za serikali
katika ujenzi wa maabara kwenye shule za serikali za kata utakaosaidia
wanafunzi wengi kupenda masomo ya sayansi na baadaye kuzalisha wataalamu
wengi zaidi nchini.
Alisema
kuwa kukosekana kwa maabara katika shule nyingi za serikali
kunasababisha wanafunzi wengi hasa watoto wakike kuogopa kuchukua masomo
ya sayansi.
Aidha, halmashauri zilizonufaika msaada huo mabati ni pamoja na Manispaa ya Iringa na Wilaya Iringa.
Awali,
Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayub alisema kuwa Mkoa wa
Iringa unahitaji jumla ya maabara 318 kwa shule 106 za sekondari mkoani,
ambapo maabara zilizopo kwa sasa ni 48 tu.
Alisema
kuwa ujenzi wa maabara katika sehemu nyingi zipo katika hatua
mbalimbali za ujenzi na kuwaomba wadau zaidi wajitokeze kusaidia juhudi
ya serikali ya kujenga maabara zaidi.
Alisema
kuwa mkuu wa mkoa kwa niaba ya ofisi ya mkuu wa mkoa iringa alikabdhi
mabati 180 kwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na mabati zingine 192
yalikabidhiwa kwa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, zenye geji ya 28.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Leticia warioba akipokea mabati
kwa niaba ya wakurugenzi wa halmashauri hizo alimshukuru mkuu wa mkoa wa
Iringa kwa juhudi yakufanyikisha ujenzi wa maabara kwa shule hizo za
wilaya.
Na Friday Simbaya, Iringa
No comments:
Post a Comment