Wananchi wa kijiji cha Kiyogo
wilayani Ludewa Katika mkoa wa Njombe wameimwagia sifa Serikali ya wilaya hiyo
kwa kuweza kuwatatulia kero ya muda mrefu ambayo ilikuwa ni ukosefu wa Zahanati
na uchakavu wa mejengo ya shule ya msingi ambayo yalihatarisha maisha ya
wanafunzi wa shule hiyo msimu wa mvua.
Akizugumza mwenyekiti wa kijiji
hicho Bw.Thomas Magnas alisema mpaka sasa tayari Zahanati yao inamganga mmoja
ambaye anafanya kazi nzuri licha ya kuwa anazidiwa na mzigo mzito wa wagonjwa
wengi lakini amekuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi hao ambao awali walikuwa
wakitibiwa katika mkoa wa Ruvuma.
Alisema awali kulikuwa na shida
kubwa kuanzia majengo ya shule ya msingi ambayo yalijengwa na shirika la
consein na kusahauliwa na Serikali pia Zahanati haikuepo hali ambayo ilikuwa ni
hatari kutokana na wananchi kuugua homa ya matumbo kutokana na uchafuzi mkubwa
wa maji ya mto Ruhuhu ambao unachafuliwa na wachimba madini.
Kijiji hicho ambacho tokea enzi za
mababu hakijawahi pata maji safi na salama ya bomba wananchi wake wamekuwa
wakiugua magonjwa ya matumbo kutokana na kutumia maji ya mto Ruhuhu ambayo ni
machafu yanayotumika na wachimba madini kuoshea madini maeneo ya wialaya ya
Mbinga na kijiji cha Amani wilayani Ludewa.
Bw.Magnas alisema Kuwa ni miaka
mingi sasa wananchi wa kijiji hicho wanakunywa maji machafu pia rangi ya maji
hayo inatisha kutokana na chanzo cha mto huo kuwepo wachimba madini wanaoyachafua
maji hayo hali hiyo imesababisha watu wengi wa kijiji hicho kupoteza maisha
kutokana na homa za matumbo lakini Zahanati imekuwa mkombozi kwa tiba
wanazozipata wananchi wa kijiji hicho.
“Tunaisifu Serikali kwa haya waliyo
yafanya maana tunayaona kwa macho yetu tofauti na awali tulikuwa tumesahaulika
kama si watanzania ila bado suala la maji kwani maji tunayoyatumia hayafai
kutumiwa na binadamu hali ambayo bado ni hatari kwa afya zetu”,alisema
Bw.Magnas.
Alisema kutokana na magonjwa ya
mripuko yanayosababishwa na uchafuzi wa maji hayo inawalazimu kwenda vijiji vya
jirani ambavyo ni Lihagule na Masasi wakati mwingine kuvuka mto Ruhuhu kwa
mitumbwi na kwenda mkoa jirani wa Ruvuma kufuata huduma za Afya lakini kwa sasa
huduma hiyo inapatikana kijijini hapo.
Licha ya kupata huduma za Afya
wananchi hao wameilalamikia Serikali kwa kutowatendea haki hasa katika suala
zima la huduma ya maji safi kwani kila siku zinavyozidi kwenda ndivyo maji ya
mto Ruhuhu yanavyozidi kuchafuliwa hali ambayo ni hatari licha ya kuwa Mbunge
wa jimbo la Ludewa Mh.Deo Filikunjombe aliahidi kulitafutia ufumbuzi suala
hilo.
Akizungumza kwa uchungu Bi.Gaudesia
Jonh alisema wamekuwa wakiyatumia maji hayo ambayo ni machafu hata ukiyaangalia
kwa rangi hali ambayo ni hatari kwa afya hasa kwa watoto wadogo ambao huugua
mara kwa mara.
Bi.Gaudesia alisema hali hiyo
imewafanya kuzarauliwa na vijiji vingine vya mkoa wa jirani kwa kutotatuliwa
kero ya maji kwa muda mrefu tokea Tanzania ilipopata uhuru mpaka sasa wakiwa ni
miongoni mwa wapiga kura wa nchi hii.
Wananchi hao wlisema bado
wanamaswali mengi vichwani mwao kama kweli Tanzania ilipata uhuru mwaka 1961 na
kusherekea miaka 50 ya uhuru huo wakati kunawananchi ambao hawana huduma muhumu
kama maji safi na salama.
Naye kaimu muhandisi wa maji wilaya
ya Ludewa,Muhandisi Marichela Maisha alisema Serikali bado iko katika mpango wa
kutatua kero hiyo hivyo bajeti ikipitishwa kijiji hicho kitapata maji safi na
salama kupitia bomba la kata ya Luilo.
Muhandisi Maisha alisema tatizo la
kijiji hicho ni kutokuwa na chanzo cha maji hivyo ni lazima utaalamu utumike
kutafuta vyanzo katika vijiji vingine ili kulitatua tatizo hilo ambalo limekuwa
kero kubwa kwa wananchi wa Kiyogo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment