Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

October 26, 2014

DIWANI WA KATA YA LUANA AWAFUNDA WAZAZI

Mh.Thomaso Haule Diwani wa kata ya Luana akiongea na wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Luana

 Mh.Thomaso akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu
 picha ya pamoja na wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari ya Luana

Mh.Thomaso akisalimiana na wahitimu

Bw.Lingalanga akiongea na wazazi katika mahafari hayo akiwa ni mlezi wa kata hiyo upande wa chama cha mapinduzi




Diwani wa kata ya Luana kupitia chama cha mapinduzi katika wilaya ya Ludewa mkoani Njombe ambaye ni makamu wa mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Mh.Tomaso Haule amewataka wazazi wa kata hiyo kutoichezea elimu na kufuatilia maendeleo yakimasomo kwa watoto wao ili kuandaa wasomi wazuri watakao fanya kazi katika migodi makaa ya mawe Mchuchu na Chuma cha Liganga.

Mh.Haule ameyasema hayo hivi karibuni katika sherehe za mahafari ya 5 ya shule ya Sekondari ya kata ya Luana ambapo alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo kwani aliona kumekuwa na uzembe mkubwa wa wazazi kutokuwa wakali kwa watoto wao hali ambayo inasababisha kuwa na maendeleo hafifu ya kimasomo kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Alisema wilaya ya Ludewa ni moja ya wilaya tajiri nchini kutokana na kuwa na raslimali za madini mbalimbali yakiwemo makaa ya mawe,Chuma cha pua,dhahabu na shaba ambayo tayari wawekezaji wameshapatikana na kazi rasmi inatarajia kuanza lakini chakushangaza bado wazazi hawana mwamko wa elimu hali ambayo ni hatari kwani migodi hiyo inahitaji wataalamu wa kufanya kazi.

Mh.Haule alisema miradi hiyo inatarajia kuajiri zaidi ya wafanyakazi 3000 na wafanyakazi hao wanatarajiwa kutoka wilayani hapa hivyo ni vyema wazazi wakatambua umuhimu wa elimu kuliko kuwa watazamaji na vibarua wakati miradi hiyo inapoanza kutekelezwa.

“Nawaomba wazazi wenzangu tujitahidi kuwasomesha  watoto wetu kwani bila kufanya hivyo tutabaki kuwa watazamaji katika ajira za migodini pindi migodi itakapoanza kufanya kazi,Serikali imepunguza ada katika shule za kata hivyo mtu unaweza kufuga kuku wawili ambao watakusaidia kupata ada pale unapowauza pia hata mtoto mwenyewe anaweza kujilipia ada kama ukimpa kuku wa kienyeji na akaanza kumfuga”,alisema Mh.Haule.

Awali akisoma lisala makamu mkuu wa shule hiyo Mwalimu Dawi Yaenda alisema ushiriki wa wazazi katika kuhakikisha wanafunzi wanakuwa na maendeleo mazuri umekuwa ni mdogo hali inayosababisha kiwango cha ufauli elimu kushuka.

Mwalimu Yaenda alisema shule hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ya nishati ya umeme licha ya kuwa shirika la Tanesco limefikisha waya shuleni hapo lakini shule haina kiasi cha shilingi milioni moja na laki sita hali ambayo shule hiyo haina uweza hivyo aliwaomba wadau mbalimbali kuchangia kiasi hicho cha pesa.

No comments: