Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

October 15, 2014

DC LUDEWA AMFUKUZA MLINZI WA NFRA KUTOONEKANA WILAYANI HAPA NA KURUDI KWAO MAKAMBAKO

Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Madaha akiongea na wakulima 
Wakulima wakimsikiliza mkuu wa wilaya wakati akimfukuza mlinzi wa NFRA

Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Ludewa Bw.Edings Mwakambonja akiongea na wakulima
Baadhi ya viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Ludewa akimsikiliza mkuu wa wilaya ya Ludewa
Mwakambonja akisisitiza jambo



               wananchi wakiwa mkutanoni

Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Solomon Madaha amemfukuza mlinzi wa wakala wa uhifadhi wa chakula nchini(NFRA)katika kituo cha manunuzi ya mahindi kilichopo Ludewa mjini kutoonekana tena wilayani hapa na kurudi kwao Mkambako kutokana na kutuhumiwa na wakulima kuwa amekuwa akifanya vitendo vya rushwa na kusababisha wakulima wadogo kushindwa kuuza mahindi yao.



Bw.Madaha alitoa amri ya kuondolewa haraka mlinzi huyo jana aliyetambulika kwa jina la Linus Mwifunye na Jeshi la Polisi wilayani Ludewa na kumrejesha katika ofisi kuu ya NFRA Makambako ili kulinda usalama wake kutokana na minong’ono ya wananchi kutaka kumdhuru mlinzi huyo kwa vitendo vyake vya kupitisha maloli ya mahindi ya wafanya biashara badala ya wakulima wadogo..



Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wakulima jana katika kituo cha Ludewa mjini ambako mpango wa Serikali wa kununua mahindi kwa wakulima unaendelea Bw.Madaha alisema amefikia uamuzi wa kumfukuza mlinzi huyo katika mji wa Ludewa kutokana na malalamiko mengi aliyoyapokea kutoka kwa wakulia hali ambayo ilikuwa inatishia usalama wa mlinzi huyo.



Alisema licha ya kuwa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutaka kununua mahindi kwa wakulima wadogo nchini lakini baadhi ya wafanyakazi wa NFRA wamekuwa si waaminifu kwani wamekuwa wakitumiwa na walanguzi na kuyapitisha mahindi ya walanguzi hao ili yaweze kuuzika na kuwaacha wakulima ambao ndio waliolengwa na mpango huo.



“alipita mkuu wa mkoa hapa na akatoa maagizo kuwa wakulima wadogo ndio wanaotakiwa kuuza mahindi yao lakini imekuwa sivyo, kwani mahindi yaliyoko hapa yalitakiwa yawe yameshapimwa  nashangaa mpaka sasa bado na kila siku upimaji unaendelea na wananchi wangu wanapingwa na jua hapa kila siku bila mafanikio kutokana na mlinzi kuingiza mahindi usiku ya wafanyabiashara hivyo kwa mamlaka niliyonayo naamuru aondoke haraka katika wilaya yangu kwa kusindikizwa na Polisi”,Alisema Bw.Madaha.



Bw.Madaha alisema hata mfumbia macho mtu yeyote atakayetaka kuwaumiza wananchi wake katika haki yao hivyo aliwataka wafanyakazi wa NFRA kufanya kazi waliyotumwa ya kununua mahindi kwa wakulima wa hali ya chini kwaajili hifadhi ya Taifa na si kuungana walanguzi katika kuwanyonya wakuliwa hao wa hali ya chini kwani ameshapata taarifa hizo za vitendo ya unyonyaji katika vituo vyote vya ununu wilayani Ludewa vinavyofanywa na maafisa wa NFRA kwa kushirikiana na walanguzi.


Naye Diwani wa kata ya Ludewa Mjini Mh.Monica Mchilo alisema malalamiko hayo ni ya muda mrefu kwani mlinzi huyo aligeuka kuwa Mungu mtu kutokana na tabia yake ya        kuwahada wakulima kwa kuwaeleza watoe hela ili waweze kupata namba ya kupima mahindi haraka bila kufanya hivyo ataendelea kuingiza mahindi ya walanguzi hali ambayo wakulima hao waliona kuwa wametelekezwa na Serikali yao.



Mh.Monica kutokana na mahindi kuwa mengi katika kituo hicho uongozi wa kijiji uliweka bango ambalo lilisitisha wakulima wengine kuleta mahindi katika kituo hicho mpaka yaliyopo yamalizike kupimwa ili kutoa nafasi ya NFRA kupanga magunia yao lakini chakushangaza mlinzi huyo na baadhi ya wafanyakazi wasio waaminifu walikaidi agizo hilo na kupitisha maloli ya mahindi nyakati za usiku.



Katibu wa umoja wa wakulima na wauzaji wa mahindi katika kituo hicho Bw.Aurelian Mhagama (AMCA) alisema bila kufika uongozi wa Serikali ya wilaya ya Ludewa kituoni hapo hali ingekuwa mbaya zaidi kutokana na mlinzi huo na baadhi ya uongozi wa kijiji kuliteka soko hilo la mahindi kwa kuwanyonya wakulima wadogo kwani jitiada  zake na viongozi wenzie ndizo zilifanya viongozi hao wafike ili kujionea hali halisi.



Bw.Mhagama alisema licha ya kuwa mlinzi huyo kuwahujumu wakulima pia hata makuli wamekuwa tatizo kubwa kwani wamepatisha bei ya ubebaji maroba ya mahindi kutoka shilingi 1000 hadi shilingi 3500 kwa roba moja lenye madebe nane kutoka umbali wa mita tano hadi kwenye mzani,hali hiyo inawaumiza sana wakulima na kukatishwa tamaa ya kuendelea na kilimo cha mahindi msimu ujao.



Alisema wakulima wengi wa hali ya chini wahana fedha kwa sasa za kumudu kulipia ubebaji huo lakini wamekuwa wakilazimishwa kulipia ubebaji kabla ya kazi kuanza na hata kama unavijana wako nyumbani wa kubeba mahindi yako ukitaka kufanya hivyo makuli hao kutoka Makambako wamekuwa wakizuia kwa kisingizio cha kuwa wao ndio wanaelewa namna ya uwekaji mahindi hayo katika mzani hali ambayo si kweli.



Bw.Mhagama aliitaka Serikali kuliangalia hilo pia kwani mpaka sasa hakuna faida yoyote anayoweza kuipata mkulima wa kawaida kwa kuuza mahindi yake zaidi ya unyanyasaji unaoendelea katika vitu vyote vya wilaya ya Ludewa toafauti na matarajio ya wakulima hao awali walipoelezwa na viongozi wa Serikali.



Aidha kamanda wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) wilayani Ludewa Bw.Edings Mwakamboja aliwataka wakulima hao katika vituo vyote wilayani huo kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa pale wanapoona kuna dalili ya vitendo vya rushwa kwani hakuna hata kituo kimoja ambacho hakina malalamiko hayo lakini ofisi yake inapojaribu kufuatilia hakuna ushirikiano kutoka kwa wakulima wenyewe.



Bw.Mwakambonja alisema ni kweli walanguzi wamekuwa wakilalamikiwa kwa kushirikiana na wafanyakazi wa NFRA lakini hakuna mkulima anayeweza kujitokeza hadharani akisema ameombwa rushwa  hivyo hakuna haja ya kuficha jambo kama wakulima hao watataka kutendewa haki katika kuuza mazao yao kwa kuhakikisha  suala hilo linakomeshwa alitoa namba yake ya simu ya mkononi kwa wananchi wote ili kumjulisha pale wanapoona kunadalili ya rushwa kwa kufanya hivyo ofisi yake itaweza kutega mtego wa kuwanasa wanaojihusisha na rushwa hizo.



Mwisho.

No comments: