Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

October 15, 2014

AFARIKI DUNIA KWA KUUNGUZWA NA MOTO KICHAA AKIWA MAWINDONI

Ndugu na jamaa wakimzika marehemu Mdanga aliyekufa kwa ajali ya moto





 Msemaji wa familia Mzee Inocent Mbawala akisoma historia ya marehemu

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Joseph Mdanga(23) mkazi wa wilaya ya Ludewa katika kijiji cha Ludewa Kijijini mkoani Njombe amefariki Dunia akiwa mawindoni kwa kuunguzwa na moto kichaa uliomzingila akiwa katikati ya msitu na kumsababishia kifo.



Msemaji wa familia ya marehemu Mzee Inocent Mbawala alisema marehemu alikumbwa na mkasa huo siku ya Jumapili ya tarehe 12/10/2014 majira asubuhi akiwa na Mbwa wake watatu alipoamua kwenda polini kwaajili ya kuwinda wanyamapoli ili kujitafutia kitoweo.



Mzee Mbawala alisema marehemu Mdanga alimuaga mchumba wake Joyce ambaye alitarajia kuoana nae kuwa anakwenda kuwinda kutokana na tabia yake ya uwindaji wanyama poli mchumba wake alimruhusu hivyo aliondoka nyumbani majira ya asubuhi akiwa na Mbwa wake watatu akielekea eneo la Lupila



Alisema ilipofika majira ya jioni mchumba wake alishangazwa kuona wanarudi Mbwa wawili bila ya mtu hali hiyo ilimfanya kuanza kutilia mashaka kwani ilikuwa si kawaida kuona wakirudi Mbwa peke yao lakini kutokana na kutomuona Mbwa mmoja akaona anaweza kuwa amepitia kwa jamaa zake.



“Marehemu amekufa kwa ajali ya moto wakati akiwa kuwinda kwani mbwa aliokuwanao mawindoni ndio waliotuonesha alipofia baada ya kupata maelekezo kwa mchumba ake kuwa alikwenda njia ya Lupila tukaamua kuwachukua wale mbwa na kuwatanguza huko na kukuta mwili wake ukiwa umeharibiwa vibaya na moto”,alisema Mbawala.



Alisema ilipofika asubihi ya siku ya pili alirudi Mbwa wa tatu bila mtu ndipo mchumba ake akaamua kutoa taarifa kwa ndugu na jamaa na kazi ya kuanza kumtafuta marehemu upande alioelekea ukaanza,juhuudi za kumtafuta zikiongozwa na Mbwa wale watatu zilizaa matunda na hatimaye kuukuta mwili wa marehemu Mdanga ukiwa umeunguzwa vibaya kwa moto.



Aidha kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Njombe Asp Fulgency Ngonyani amethibitisha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kifo cha Joseph Mdanga kwa kuunguzwa na moto hivyo jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi zaidi kujua ni nani aliyesababisha moto huo.



Naye mwenyekiti wa Ludewa kijijini Bw.Disbod Haule amewataka vijana wa kijiji hicho kuacha tabia ya kuwinda kwa mtu mmoja mmoja bali wanatakiwa kuwa wengi ili kupeana ushirikiano pale wanapopatwa na matatizo wawapo mawindoni hasa katika maeneo ya mbali na kijiji hicho.



Mwisho.








No comments: