Msemaji wa familia Mzee Inocent Mbawala akisoma historia ya marehemu
Mtu mmoja aliyefahamika kwa
jina la Joseph Mdanga(23) mkazi wa wilaya ya Ludewa katika kijiji cha Ludewa
Kijijini mkoani Njombe amefariki Dunia akiwa mawindoni kwa kuunguzwa na moto
kichaa uliomzingila akiwa katikati ya msitu na kumsababishia kifo.
Msemaji wa familia ya marehemu
Mzee Inocent Mbawala alisema marehemu alikumbwa na mkasa huo siku ya Jumapili
ya tarehe 12/10/2014 majira asubuhi akiwa na Mbwa wake watatu alipoamua kwenda
polini kwaajili ya kuwinda wanyamapoli ili kujitafutia kitoweo.
Mzee Mbawala alisema marehemu
Mdanga alimuaga mchumba wake Joyce ambaye alitarajia kuoana nae kuwa anakwenda
kuwinda kutokana na tabia yake ya uwindaji wanyama poli mchumba wake alimruhusu
hivyo aliondoka nyumbani majira ya asubuhi akiwa na Mbwa wake watatu akielekea
eneo la Lupila
Alisema ilipofika majira ya
jioni mchumba wake alishangazwa kuona wanarudi Mbwa wawili bila ya mtu hali
hiyo ilimfanya kuanza kutilia mashaka kwani ilikuwa si kawaida kuona wakirudi
Mbwa peke yao lakini kutokana na kutomuona Mbwa mmoja akaona anaweza kuwa
amepitia kwa jamaa zake.
“Marehemu amekufa kwa ajali ya
moto wakati akiwa kuwinda kwani mbwa aliokuwanao mawindoni ndio waliotuonesha
alipofia baada ya kupata maelekezo kwa mchumba ake kuwa alikwenda njia ya
Lupila tukaamua kuwachukua wale mbwa na kuwatanguza huko na kukuta mwili wake
ukiwa umeharibiwa vibaya na moto”,alisema Mbawala.
Alisema ilipofika asubihi ya
siku ya pili alirudi Mbwa wa tatu bila mtu ndipo mchumba ake akaamua kutoa
taarifa kwa ndugu na jamaa na kazi ya kuanza kumtafuta marehemu upande
alioelekea ukaanza,juhuudi za kumtafuta zikiongozwa na Mbwa wale watatu zilizaa
matunda na hatimaye kuukuta mwili wa marehemu Mdanga ukiwa umeunguzwa vibaya
kwa moto.
Aidha kamanda wa jeshi la
Polisi mkoani Njombe Asp Fulgency Ngonyani amethibitisha amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo la kifo cha Joseph Mdanga kwa kuunguzwa na moto hivyo jeshi la
Polisi linaendelea na uchunguzi zaidi kujua ni nani aliyesababisha moto huo.
Naye mwenyekiti wa Ludewa
kijijini Bw.Disbod Haule amewataka vijana wa kijiji hicho kuacha tabia ya
kuwinda kwa mtu mmoja mmoja bali wanatakiwa kuwa wengi ili kupeana ushirikiano
pale wanapopatwa na matatizo wawapo mawindoni hasa katika maeneo ya mbali na
kijiji hicho.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment