Bw.Nyangasa akiangalia shughuri za ununuzi wa mahindi
Diwani wa kata ya Ludewa Monica Mchilo akiongea na wanahabari
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Kapten
mstaafu Aseri Msangi amewataka wakulima mkoani hapa kuwa na utamaduni wa kusafisha
mahindi yao na kuyatunza kwa uangarifu kabla ya kuyauza kwa wakala wa hifadhi
ya chakula ya Taifa.
Kapten Msangi aliyasema hayo
jana wakati wa ziara yake ya kikazi katika vituo vya ununuzi wa mahindi
wilayani Ludewa ambako wakala wa hifadhi ya chakula Taifa(NFRA)wananunua
mahindi ya wakulima.
Alisema ifike wakati wakulima
wawe na utamaduni wa kuuza mahindi masafi kwani Serikali inapata hasara kubwa
kwa kununua mahindi machafu na yasiyo na viwango ambayo yatakataliwa katika
soko la kimataifa na nchi jirani.
Aliwataka wasimamizi wa
manunuzi kuangalia zaidi wakulima wa hali ya chini ambao wametumia mitaji yao
yote katika kilimo kwani yasiponunuliwa mahindi yao hali ya kiuchumi itazidi
kuwa mbaya zaidi tofauti na wale wakulima wakubwa ambao wanaweza kuyasafirisha
mahindi hayo hadi nchi jirani.
“nawaomba ninyi mliopewa
dhamana na Serikali ya kuyanunua mahindi haya myanunue yakiwa masafi na yenye
ubora ili yauzike kimataifa pia hawa wakulima wadogo ndio wanaotakiwa kuanza
kuyauza mahindi yao kwenu na si hawa wenye roba zaidi ya 600 kutokana na ukweli
usiopingika kuwa hawa wengine wanauwezo wa kuyasafirisha lakini hawa wadogo
hawana uwezo huo’’,Alisema Kapten Msangi.
Kapten Msangi aliyasema hayo
kutokana na uzalishaji mkubwa wa mahindi nchini kwa mwaka huu tofauti na
kiwango cha ununuzi wa mahindi hayo kilichopangwa na Serikali hivyo bila
kuwasaidia wakulia wadogo basi wimbi la umaskini litakuwa kubwa nchini.
Aidha meneja wa hifadhi ya
chakula ya Taifa(NFRA) kanda ya nyanda za juu kusini kituo cha Makambako(NFRA)Bw.Abdilla
Nyangasa alisema Serikali imetoa fedha za kununulia mahindi kwa wakulima na
kuacha mambo mengine hivyo wasimamizi wa vituo vya ununuzi wanapaswa kuzitendea
haki fedha hizo kwa kununua mahindi yenye ubora.
Bw.Nyangasa alisema kinachotakiwa
kwa wakulima ni kuleta mahindi masafi ili yaweze kuuzika katika mataifa mengine
yenye shida ya chakula kwani baadhi ya wakulima wamekuwa wanatabia ya kuuza
mahindi machafu wakiamini NFRA watafanya kazi ya kuyasafisha hali ambayo si
sahihi.
Alisema wakulima wakitanzania
wanapaswa kuanza kujifunza namna ya kuhifadhi chakula ambacho kitaweza kuuzika
katika mataifa mengine na si kuishi kwa mazoea kwakufanya hivyo wakulima
wanaweza kujiingizia fedha nyingi za kigeni na kuachana na umaskini
uliokithiri.
Bw.Nyangasa alisema hata sita
kumfukuza kazi mfanyakazi yeyote wa NFRA
ambaye itathibitika kuwa aliruhusu kupima mahindi machafu kwa kupewa
rushwa na mkulima mkubwa kwani kwa kufanya hivyo atakuwa amekiuka misingi ya
kazi aliyopewa kuifanya na Serikali.
Alisema katika kanda ya
Makambako ni tani elfu arobaini tu ndizo zilizopangwa kununuliwa na Serikali
hivyo wasimamizi wa manunuzi wanatakiwa kuwa makini kutokana na hali halisi ya
uzalishaji mkubwa wa mahindi kwa mwaka huu hali hii inaweza kusababisha mianya
ya rushwa kwa wanaotaka kutangulia kupima mapema mahindi yao.
Bw.Nyangasa aliwaomba wakulima kushirikiana na
viongozi wa wilaya katika kufichua mambo yote ambayo si sahihi yanayofanywa na
wasimamizi wa manunuzi katika vituo na kutoa taarifa mapema katika vyombo
husika pale wanapoona kuna harufu ya rushwa.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment