Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

September 08, 2014

LUDEWA RANGERS TIMU KONGWE INAYOENDELEA KUSAKATA KABUMBU KATIKA LIGI YA MBUZI WILAYANI LUDEWA

Hawa ndio vijana wa timu kongwe wilayani Ludewa wakiendelea kuienzi Ludewa Rangers ambayo inashiriki mashindano ya Kombe la Mbuzi yanayofanyika Ludewa Mjini


Mwamuzi Bw.Bazil Makungu akiongea na vijana wa Timu ya Ludewa Rangers wakati wakikaguliwa

Timu ya Ludewa Rangers ilianzishwa miaka 30 iliyopita ikihusisha wachezaji ambao ni wanafunzi na mpaka sasa imeendelea na utaratibu huo ikiwa na muanzilishi

Viongozi wa Timu hiyo wakijadiliana jambo wakiti kabumbu likiendelea uwanja wa Ludewa Mjini
Vijana wa Ludewa Rangers wakiwa na Furaha kabla ya kulianza Pambano
Ludewa Rangers wakiwa ukimenyana na Vijana Stars katika uwanja wa wilaya ya Ludewa
Mwamuzi wa pembeni Sadiki Nyaulile akiwa kazini katika mchezo huo

TIMU ya Ludewa Rangers ni timu kongwe wilayani Ludewa ilianzishwa miaka 30 iliyopita ikiwa chini ya mwalimu Mnyawasa na ikifadhiriwa na Mzee Chorobi ambaye baadae alihamia mjini Iringa na kuiacha timu hiyo ikiwa chini ya mtaa wa Mkondachi ikijulikana kama watoto wa mama Limbala ambaye alikuwa mwenyekiti wa mtaa wa Mkondachi.

Timu hiyo imeendelea kuzarisha wachezaji ambao wamekuwa wakichukuliwa na timu mbalimbali kutokana na uhalisia wa timu hiyo kuwa ni timu inayozalisha wazezaji hasa walioko mashuleni ambao ndio wamekuwa wachezaji wa timu hiyo ya mpira wa miguu yenye makao yake makuu mtaa wa Mkondachi katika kata ya Ludewa.
Hivi sasa timu ya Ludewa Rangers inashiriki Ligi ya Mbuzi ambayo imeanzishwa na Mh.Hakimu wa wilaya ya Ludewa Fledrick Lukuna na kupata udhamini wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Wilayani Ludewa ambao wameweza kutoa zawadi ya Mbuzi mmoja,Mh.Lukuna almetoa Mbuzi mmoja na Fransis Luoga ametoa Mbuzi mmoja.

Lengo likiwa kukuza vipaji kwa vijana na kutoa ujumbe na taadhari ya mapambano dhidi ya Rushwa hasa pale ambapo kabla au baada ya mchezo kuanza ili kuhakikisha jamii ya Ludewa inakuwa na uelewa sahihi kuhusiana na Rushwa.

Endelea kufuatilia mtandao huu ili ipate habari zaidi.

No comments: