MTUNZI; Moringe Jonas
MAWASILIAANO; Jonasymoringe@gmail.com
SEHEMU YA TATU
KWA WASOMAJI WAPYA;
Delphine anashuhudia wazazi na ndugu zake wakiuawa kikatili
na watu wa kabila tofauti na lake nchini Rwanda
kupitia nafasi kitundu kidogo
kilichokuwa chooni alipoelekea mara tuu
baada ya kuamka.Anaamua kukimbia ambako hakujua alikoelekea zaidi ya
kupotelea katika msitu mkubwa uliokuwa
mashariki mwa nchi ile uliokuwa ukiziunganisha nchi za Rwanda ,Burundi na
Tanzania ambako anaokotwa na watu walioenda kutafuta ngozi ya joka lililokuwa
humo kwa kile kilichodaiwa wangepata utajiri.
Joka hilo la ajabu
linasababisha vifo vya baadhi yao kiajabu ajabu hali iliyowafanya watu
wale kupoteana baada ya joka lile kuuawa
lakini baadaye linajitokeza , safari hii watu wakionekana kuliabudu.
Baada ya safari hiyo
iliyokuwa na mikasa ya ajabu iliyopelekea
pia kifo cha mganga
aliyewatuma kuifuata Ngozi hiyo kinawashtua na kulivuruga kabisa kundi lile
la marafiki na kubadili kabisa mfumo wa maisha wa watu wale.
Miaka ilipita
hatimaye Delphine anakuwa binti mkubwa aliyeanza kuwavutia
wavulana wa rika lake na hata wakubwa baada ya malezi aliyoyapata kutoka
katika jamii ya akina Mwita ambaye alimuokoa kule porini.Lakini jambo la ajabu
linatokea katika maisha yake ya kujifunza ukunga ambapo alitakiwa kufanyiwa tohara kama jamii
ile ilivyomtaka. Anakimbilia kwa Mwita ambaye alimwona kama mzazi wake huko nako anagundua kuwa malengo
ya kulelelwa yalikuwa kuolewa na Yule baba jambo limfanyalo akimbilie mbugani kulikokuwa na hatarui kubwa
ya kuliwa na wanyama wakali.
Kwenye kibarabara
kisichoeleweka mbugani anashtushwa na
sauti ya kutisha ambayo kadiri muda ulivyopita iliongezeka na kumfanya akose la
kufanya.
SONGA NAYO………..
Gari dogo la kitalii
lilionekana kwa mbali kilima na kumfanya Delphine apate tumaini jipya kwani
akili yake ilimwaminisha ilikuwa ni sauti ya simba.Alijiweka vizuri kuomba
msaada lakini alama ya michilizi ya mkojo uliotokana na hofu zilishindwa
kufichika.
‘’We binti huogopi hapa porini?’’aliuliza baba mmoja mara baada lile gari kusimama.
‘’Nina matatizo makubwa hapa nilipo baba yangu’’Aliongea
Delphine akiangalia garini ambako kulikuwa na watu wasabi huku dereva aliwa ni
mwafrika pekee wengine wote wakiwa wazungu.
‘’Haya panda gari haraka tukupeleke sehemu salama’’Alimrisha
Yule baba akianza kuelekea garini.
Gari dogo la kitalii
lilionekana kwa mbali kilima na kumfanya Delphine apate tumaini jipya kwani
akili yake ilimwaminisha ilikuwa ni sauti ya simba.Alijiweka vizuri kuomba
msaada lakini alama ya michilizi ya mkojo uliotokana na hofu zilishindwa
kufichika.
‘’We binti huogopi hapa porini?’’aliuliza baba mmoja mara baada lile gari kusimama.
‘’Nina matatizo makubwa hapa nilipo baba yangu’’Aliongea
Delphine akiangalia garini ambako kulikuwa na watu wasabi huku dereva aliwa ni
mwafrika pekee wengine wote wakiwa wazungu.
‘’Haya panda gari haraka tukupeleke sehemu salama’’Alimrisha
Yule baba akianza kuelekea garini.
Delphine alipanda
kwenye lile gari la kitalii na kukaa kwenye moja ya siti zilizokuwa garini
akiwaacha wale wengine wakiwa wamesimama wakiendelea kupiga picha wanyama na miti iliyoonekena kama muhimu sana
kwao kwa wakati ule kwani ndicho kilichowapeleka kule porini.
Hakukuwa na mzungu
hata mmjoja aliyejishughulisha na Yule msichana zaidi ya kumsikiliza Yule mtu aliyekuwa akiwaeleza kuhusu mambo mbalimbali waliyoyaona kila walipopita.
Katikati ya
mazungumzo hayo ambayo lugha ya
kifaransa ikitawala , ambapo maneno machache tuu yalipata maana kwenye ubongo
wa Delphine amabaye alishtuka kila alipowaona simba. Aliwaza kama angeendelea
kutembea mle mbugani peke yake kama
angefanikiwa kutoka salama kwenye mbuga
ile iliyokuwa kubwa sana Afrika
Mashariki.
Taswira ya ndugu zake wakiuawa ilijirudia akilini mwake na
kujikuta akitoa machozi na hakujua
sababu iliyomfanya awakumbuke wakati ule kwani alikuwa hajawakumbuka kwa
muda mrefu kufikia hatua ya kutoa machozi.Ilitokea mara chache sana kwake kuwalilia wazazi wake waliokuwa wamepoteza
maisha miaka zaidi ya kumi iliyopita na
kila alipofikia hatua hiyo alitamani kurudi
tena Rwanda kulipiza kisasi juu ya mambo yaliyotokea kipindi kilichopita.Aliwachukia sana watu
wale akiapa kutowasamehe milele wale
watu kwani aliamini hata kwa toba ipi wasingesamehewa hata
na Mwenyezi Mungu.
Alijua wao ndio waliosababisha awe katika hali ile ya
kukimbia kimbia , tena akiwakimbia wanadamu wenzake ambao kila mmoja hakuwa
nania njema kwani wakati akikimbia kukeketwa anakutana na jambo jipya la kutaka
kuolewa na mwanaume ambaye kwake alikuwa
ni kama baba yake.Yote hayo yalitokana uhasama wa kikabila uliochochewa na
siasa chafu nchini mwake, alitamani kuona siku watu wale wakiadhibiwa kwa
mateso makali ambayo huenda yangekuwa ni pozo la moyo wake.
Gari la kijani aina
ya LAND CLUISER lilisimama mbele ya jengo moja ambalo lilionekana ndiyo mwisho wa safari ya watu
wale waliokuwa garini waliomtaka
Delphine ashuke pamoja nao.
Walipofika ndani ya jengo lile waliletewa chakula huku
Delphine akihimizwa na kila mmoja kula na baada ya kula alipewa mavazi ambayo
alitakiwa kuyavaa baada ya kuoga kwani mavazi aliyotoka nayo kijijini yalikuwa
kmachafu sana. Mavazi yale yalifanamna na mavazi waliyovaa wafanyakazi
waliokuwa wakifanya kazi ya upishi katika nyumba ile iliyokuwa ni hoteli ya kitalii, jambo lililomshangaza
Delphine kwani awali aliamini kuwa ni watalii tuu sasa ilikuwaje wampe mavazi
yaliyokuwa sare za wapishi wa iile
hoteli ya kitalii.
‘’Unaitwa nani?’’Lilikuwa ni swali la kwanza alililoulizwa Delphine mara tuu alipoketi kitini baada ya kuoga na kubadili zile nguo zilizomfanya aonekane kama
mmoja wa wapishi wa ile Hoteli.
‘’Delphine Mwita’’alijibu huku akionekana kuwa na uoga wa ajabu kwani alijikuta akiamua
kuwadanganya wale watu ili apate msaada.
‘’Umetokea wapi na
kwa nini ulikuwa pale porini?’’Aliuliza maswali
mfulizo Yule mtu huku akionekana kuwasikiliza sana na kuwaelekeza wale watalii wa kizungu .
‘’Nimetokea Mugumu
huko walitaka wanikekete na
kunioa katika umri huu mimi yatima jamani’’Aliongea Yule binti akitoa
nkilio cha hisia kilichowafanya wale watu wamhurumie sana kabla hata ya kuelekezwa maana ya
alichokiongea na yule aliyeonekana kama mkalimani wao.
Baada na maelezo
mengi yaliyojaa uongo uliokuwa wa
kiwango cha juu kufikia hatua ya kumtoa machozi mama mmoja ambaye alionekana
naye kama ana mamlaka Fulani kwenye ile
hoteli kutoa machozi akimtaka amshukuru
sana mungu kwa kumwepusha na mauti
akiwa mbugani , mbuga ambayo ilikuwa
na wanyama wengi hatari kwa maisha ya wanadamu hata wanyama
wenzao.
Baadaye alitakiwa
kulala na mmoja wa wapishi wa hoteli ile huku wakiahidi kumpa msaada alioumba ambao ulikuwa ni kuwa
mbali juu ya watu wale waliotaka kumfanyia mam,bo ambayo hakupenda kabisa
yatokee kwake.
Uchovu na kilio cha
jioni ile vilimfanya Delphine apate usingizi mapema sana mara tuu alipojitupa
kitandani akimwacha mwenzake aliyetakiwa
kulala naye akihanagaika hangaika mle ndani na pilika zilizokuwa hazina maana,
mara akashike chanuo mara ajaribu gauni mara akwangue kucha za miguu ili mradi tuu hatulii.Usiku wa manane
Delphine alishtuka kutoka usingizini baada ya kuota ndoto Fulani ya kutisha
ambayo Marehemu Mama yake alimtokea
ndotoni akimwambia kuwa wale watu
aliokuwa nao hawakuwa wema hata kidogo ajitahidi kuondoka pale mapema sana
kabla mabo mabaya hayajamtokea.
Alipoangalia Pembeni
yake ambapo Yule mwanamke aliyeambiwa angelela
naye hakuona chochote zaidi ya
shuka lililokuwa kimekunjwa kana kwamba
kakukuwa na mtu aliyelala pale.
‘ Aliogopa’, hasa kutokana na ile ndoto ambayo ilimhusisha
mtu aliyefariki miaka mingi iliyopita , tena
hakuwahi kumwota hata siku moja tangu alipouawa kinyama na wale
watu.Alianza kupata hofu juu ya wale watu ambao hakujua walikuwa na kazi gani japo walionekana kama
watalii lakini walikuwa na mamlaka sana
tofauti na walivyokuwa watalii wengine
waliokuwa pale hotelini.
Akiwa katika kutafakari juu ya mambo hayo alishtushwa na
sauti ya hatua zilizokuwa zikionekana zikielekea katika chumba kile alichokuwa amelala, wazo
la haraka lilimjia akijamini kuwa alikuwa ni Yule rafiki yake waliopangwa kulala pamoja.
Bila kutarajia alijikuta anachukua uamzi wa kusimama na
kujificha nyuma ya kabati la nguo
lililokuwa mle ndani , na Yule mtu
alipoingia alikuwa ni mtu ambaye alimfanya ashindwe kuelewa sababu iliyompeleka pale ndani muda ule.
Alikuwa ni mmoja wa
wale watu aliosafiri nao wakitokea Mbugani akiwa ndiye Dereva wao , ambaye moja
kwa moja alienda kitandani kujilaza na kujifunika ile shuka iliyokuwa imekunjwa
pale pembeni ya alipolala Delphine .
Akiwa nyuma ya ile kabati ndogo Delphine alitetemeka sana
baada ya kuona Yule mtu akiamka na kuanza kuangaza huku na huko mle ndani kabla
ya kutoka nje ya kile chumba.Yule mtu alirudi muda mfupi baadaye akionekana
bado akitafuta kitu mle ndani
jambo ambalo Delphine alilinganisha na ndoto aliyokuwa ameiota.
ITAENDELEA……………
Je , Yule mtu alifuata nini ?
Yupi ni mama muuaji?
No comments:
Post a Comment