washiriki wa warsha wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza mafunzo
Wawezeshaji wakijadiliana jambo kabla ya kuanza mafunzo
washiriki wakimsikiliza wezeshaji
Shirika la Mlangali Development
Association(MLADEA) lenye makao yake makuu katika kata ya Mlangali
wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe kwa kushirikiana na Halmashauri
ya wilaya ya Ludewa kupitia ufadhiri wa The foundation for civil
society wameandaa mpango mkakati utakaoweza kuwasaidia watoto
wanaoishi katika mazingira hatarishi wilayani hapa.
Akisoma taarifa ya maandalizi ya mpango
mkakati huo mratibu wa shirika la MLADEA Bw.Emmanuel Kayombo alisema mradi huo
wa kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi
utatekelezwa katika tarafa ya mawengi wilayani hapa kutokana na
takwimu ya watoto hao kuwa juu tofauti na tarafa nyingine.
Bw.Kayombo alisema wilaya ya Ludewa
ambayo ilianzishwa rasmi Novemba 28 mwaka 1975 na kuwa Halmashauri ya
wilaya Julai 1mwaka 1984 kwa sheria namba 5 ya Serikali za mitaa,sura
ya 287 na kufanyiwa marekebisho yake mwaka 2002 ina jumla ya tarafa 5
kata 25,vijiji 77 na vitongoji 340 ina jumla ya watu 133281.
Alisema kulingana na taarifa ya sensa
ya watu na makazi ya mwaka 2012 inaonesha kuwa tarafa ya Mawengi ina
jumla ya watu 23768 ikiwa me 13721 na ke 10047 ambapo tarafa ina
jumla ya kata 3 na vijiji 10 hivyo bado kumekuwa na uelewa mdogo kwa
wananchi kuhusiana na sera na sheria mbalimbali ikiwemo sera na
sheria ya haki za mtoto hali inayosababisha kushindwa kuthaminiwa.
“Asasi za kiraia kwa kushirikiana na
halmashauri ya wilaya ya Ludewa tungependa kuwa na wananchi wenye
maisha bora na endelevu ifikapo mwaka 2025 hivyo ni wajibu wa asasi
zote kuandaa mipango mikakati kwa kushirikiana na wafadhiri ili kutoa
elimu kwa wananchi katika kuandaa kamati za watoto wanaoishi katika
mazingira hatarishi kwa kila kijiji na mitaa ambazo zitawasaidia
watoto hawa ambao wametelekezwa”,alisema Bw.Kayombo.
Bw.Kayombo alisema jamii ya tarafa ya
Mawengi imekuwa haiwathamini watoto wanaoishi katika mazingira
hatarishi kutokana na ukosefu wa elimu hali ambayo itasababisha kuwa
na waharifu wengi kutokana na kutothaminiwa na jamii inayowazunguka.
Aisha mwezeshaji wa mpango huo ambaye
ni ofisa maendeleo ya jamii katika halmashauri ya wilaya ya Ludewa
Bw.Thomas Kiowi alisema ifike wakati jamii inapaswa kutambua watoto
hao ni miongoni mwa wanajamii kwani wakithaminiwa na kuendelezwa
wanaweza kuwa viongozi wazuri kutokana na hali halisi ya maisha yao
wanavyoishi.
Bw.Kiowi alisema imekuwa kawaida katika
jamii kuona watoto hao ni mali ya Asasi za kiraia na wafadhiri hali
ambayo si kweli hivyo kupitia kamati za watoto wanaoishi katika
mazingira hatarishi watoto hao ni mali ya jamii na jamii inapaswa
kuwasaidia watoto hao katika michango mabalimbali ikiwemo ya mavazi
na chakula kama wanavyoishi watoto wengine.
Alisema kuna baadhi ya maeneo tayari
jamii imehamasika kutokana na kupata elimu hivyo tayari kila familia
au kaya imekuwa ikitenga chakula na bajeti nyingine kwaajili ya
watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi kwa kupitia kamati
zilizochaguliwa na wanajamii wenyewe hali ambayo inatia moyo na
watoto hao wanaishi maisha ya kawaida kutokana na kuthaminiwa.
Bw.Kiowi aliwataka wanajamii wa tarafa
ya Mawengi kwa kushirikiana na shirika la Mladea kuunda kamati hizo
haraka ambazo zitasimamia na kutoa elimu kwa wananchi namna ya
kuwasaidia watoto hao hata kama wafadhiri watasitisha misaada yao
lakini jamii itakuwa na uwezo wa kuwaendeleza kielimu na huduma
nyingine.
No comments:
Post a Comment