Filikunjombe akipata maelezo kutoka kwa mtaalam wa TANROAD
Mkurugenzi wa GS CONTRUCTORS CO.LTD akipokea mkataba
Mbunge wa
jimbo la Ludewa katika mkoa wa Njombe Deo Filikunjombe ameanza kuwabana
Makandarasi wanaofanya upanuzi wa barabara ya
Itoni,Mkiu,Liganga na ile ya Mkiu,Ludewa hadi Nchuchuma kwa kufanya
ukaguzi wa kushitukiza ili kubaini changamoto wanazokabiliana nazo.
Katika ukaguzi
huo aliweza kujionea baadhi ya makandarasi ambao wanafanya vizuri na kwenda na
muda waliopangiwa katika mkataba na wengine kushindwa kufanya kazi kwa wakati
kutokana na uchakavu wa mitambo wanayoitumia hali ambayo iliwafanya kushindwa
kujitetea walipotakiwa kujieleza kwanini hali imekuwa tofauti na mkataba.
Barabara
hizo zinajengwa kwa gharama ya shilingi 7.8 bilioni ambazo katika mkataba
makandarasi walipewa muda wa mienzi miwili kufanya upanuzi huo ili mitambo ya
wawekezaji wa miradi ya makaa ya mawe
Nchuchuma na chuma cha Liganga zinatakiwa kuisha mapema ili kuleta
chachu ya maendeleo wialayani Ludewa.
Barabara hizo ni zile za Itoni Mlangali ambayo amepewa
Boimanda modern CO.LTD,Mlangali hadi Ludewa inajengwa na Mtwivila Traders
Contruction CO.LTD,Ludewa hadi Ngomang'ombe,Mchuchuma inajengwa na G;S
Contractors CO.LTD na ile ya Mkiu hadi Liganga inajengwa Canopies
International(T)LTD.
Filikunjombe amewaonya na kuwataka makandarasi
wazarendo wanaofanya kazi ya kupanuzi wa
barabara ya Itoni hadi Ludewa kuwa waaminifu na waadilifu vinginevyo hatasita
kuomba mwongozo wa spika kwa yeyote atakayekwenda kinyume na mkataba.
Filikunjombe
aliwataka Makandarasi hao kufanya kazi kama walivyosaini mikataba yao ili
kujiletea sifa kwa makandarasi wazawa kwani kwa kufanya hivyo wanaweza
kuaminiwa na Serikali yao hali ambayo itawasaidia kupata tenda nyingi nchini na
kuweza kujitangaza zaidi.
“mimi
nawahakikishieni kuwa kazi hii ya Ludewa inaweza kuwapa sifa kubwa mkiifanya
vizuri na inaweza ikawaweka pabaya kama mtashindwa kuifanya kwa kiwango
kinachokubalika hivyo wananchi wa Ludewa hawata kubali kuona fedha za Serikali
hazifanyi kazi iliyopangwa ninawaomba ifanyike kwa muda uluiopangwa”,alisema
Filikunjombe.
Alisema
wilaya ya Ludewa inachangamoto kubwa ya miundombinu hali inayowafanya vijana
kukimbilia mjini kwa lengo la kuatafuta amaisha lakini kwa kasi hii ya Serikali
inayoongozwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete vijana walio wengi wataweza kurudi
na kuishi wilayani hapa.
Aidha
mkurugenzi wa G,S Contructors Bw.Seven Gamba ambaye kampuni yake inakarabati
barabara ya Ludewa mjini hadi Nchuchuma alimsifu Filikunjombe kwa ufuatiliaji
wake kwani kwa kufanya hivyo wakandarasi wazawa watafanya kazi kwa umakini
mkubwa tofauti na zamani walikuwa wakibweteka.
Bw.Gama
alisema licha ya mitambo yake kuwa mibovu mara kwa mara lakini amejifunza kitu
kikubwa kutoka kwa filikunjombe ambacho kinahitaji utekelezaji wa haraka hivyo
atajitahidi kuimaliza kazi kwa muda uliopangwa ili kuweza kujizolea sifa ambazo
zitamsaidia kupata kazi kubwa zaidi.
Aliwataka
makandarasi wengine kufanya kazi kwa juhudi na uaminifu mkubwa kama
alivyowaelekeza Filikunjombe kwani mbunge huyo anania nzuri na makandarasi
wanaofanya kazi katika wilaya ya Ludewa ambao mpaka sasa baadhi wako katika
hatua nzuri ya utendaji kazi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment