BRAZIL NA CHILE, UHOLANZI NA MEXICO RAUNDI YA PILI

Neymar
alifunga mara mbili katika mechi aliyokuwa mchezaji bora wakati Brazil
ilipoishinda nguvu Cameroon na kufuzu katika raundi ya muondoano.
Mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 22 alifunga mabao 2 katika kipindi cha kwanza
baada ya bao la kusawazisha lake Joel Matip, huku Fred na Fernandinho
wakihakikishia timu hiyo nafasi katika mkondo wa pili wa timu 16 bora
kama washindi wa kundi A.
Matokeo duni
dhidi ya Croatia na Mexico yameibua wasiwasi kuhusu Brazil - na hofu
inasalia katika safu yao ya ulinzi - lakini Neymar akiwepo, chochote
chaweza kutokea.Kushiriki kwa Brazil katika robo fainali kunategemea
mechi yao dhidi ya Chile katika robo fainali, na Brazil watakwenda
katika mechi hiyo itakayochezewa jijini Belo Horizonte siku ya Jumamosi
wakiwa na imani mpya ya kunyakua taji hilo.
Mshambulizi
huyo wa Barcelona alirejea na bao dhidi ya Japan katika mechi ya
ufunguzi katika mechi ya kwanza ya Kombe la Mashirika la mwaka uliopita,
ambayo iliisaidia Brazil kuanza kwa ushindi ili kunyakua taji hilo, na
kocha Luiz Felipe Scolari atatumai kuwa matokeo haya yatakuwa na athari
sawa.

Scolari alitaja kikosi
sawa na kile kilichoishinda Japan, kumaanisha kuwa Hulk alirejea kutoka
kwenye jeraha na kuchukua nafasi yake Ramires katika mfumo wa 4-3-3,
sawa na ulioishinda Croatia.
Brazil
ilikuwa karibu kupata bao la kwanza mkwaju wake Paulinho ulipozuiliwa
baada ya Hulk kumpigia pasi iliyokuwa imetoka kwake Neymar, lakini tamaa
yao ya kushambulia ikawafanya kusahau safu ya ulinzi, ambayo Cameroon
ilonekana kutaka kutumia.
Marcelo
aliokoa mkwaju ambao angefunga Vincent Aboubakar kabla ya David Luiz
kulazimika kuondoa mkwaju aliokuwa ameupiga Eric Choupo Moting katika
eneo la lango.
Hata hivyo,
Brazil walionekana wasiokata tamaa, Luiz Gustavo alipata mpira katika
ubavu wa kushoto na kumpigia pasi Neymar ambaye alimpiku Charles Itandje
na kufunga bao.
Ilikuwa njia
nzuri ya kuandikisha bao la 100 katika Kombe la Dunia - na mchezaji
yuyo huyo alikaribia kufunga bao la pili ambalo Itandje aliondoa.
Uwanja
uliokuwa umejaa kelele ulinyamaza kimya wakati Cameroon walipoweka wazi
safu hafifu ya ulinzi ya Brazil, Nyom akimpiku Dani Alves na kumpigia
pasi Matip aliyefunga kwa karibu.
Scolari
aliwaashiria wachezaji wake, nao wakamjibu kwa njia ya pekee wanayojua,
Marcelo kumpigia Neymar pasi ambaye alikimbia na kuwapiga chenga mabeki 2
wa Cameroon na kufunga bao lake la 35 katika mechi 52 za kimataifa.

Brazil ilitamatisha mechi za kundi kwa kishindo iliilaza Cameroon 4-1
Scolari alimwondoa Paulinho na kumweka Fernandinho wakati wa mapumziko .
Kiungo huyo wa Manchester City alichangia nipe nikupe iliyozaa bao lake Fred .
Fernandinho alifunga bao la nne na kuonyesha kuwa kuwepo kwake kulichangia ushindi huo.
Katika hatua
nyingine, Uholanzi ilimaliza katika nafasi ya kwanza kwenye kundi B
kufuatia ushindi wa mabao 2-0 katika mechi yao ya mwisho ya makundi.
Mabao ya
Uholanzi yaliyofungwa na Leroy Fern na Memphis Depay yaliyowapa ushindi
dhidi ya Chile katika mechi ngumu iliyochezewa jijini Sao Paulo.
Mechi hiyo
ilikosa msisimko na kuishia sufuri bin suifuri kufikia muda wa
mapumziko ,Lakini Fer alifunga kwa kichwa katika dakika ya 77, kabla ya
Depay kufunga katika dakika ya mwisho.Timu
zote mbili zilikuwa tayari zimefuzu kwa raundi ya pili baada ya
kushinda mechi zao za kwanza dhidi ya Uhispania na Australia.
Huenda Chile
wakachuana na Brazil katika mechi za muondoano, huku upande wa Luiz Van
Gaal ukitarajia kuchuana na aidha Mexico au Croatia.
Uholanzi ilikuwa bila mshambulizi Robin Van Persie ambaye alikuwa anatumikia marufuku baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano.

Uholanzi kuvaana na Chile mkondo wa pili
Chile nayo
ilimpumzisha kiungo cha kati Arturo Vidal ambaye kukosekana kwake
kuliadhiri mchezo, kwani ilichukua muda kabla ya walinda lango kuugusa
mpira.
Mshambulizi
wa Barcelona Alexis Sanchez alionekana kutaka kufunga bao la kwanza kwa
Chile kwa weledi wake na pasi ambazo ziliwahangaisha mabeki wa Uholanzi
kwa muda.
Arjen Robben alikuwa karibu kuendeleza rekodi yake ya kufunga bao katika kila mechi baada ya mkwaju wake kukosa lango.
Ilikuwa hadi dakika ya 65 wakati mlindalango Jasper Cillessen alipolazimika kuokoa mkwaju wa Sanchez uliopigiwa karibu na lango.
Hilo
liliwatia waholanzi motisha na kumfanya Robben kupiga mkwaju uliomlenga
Claudio Bravo katika lango la Chile baada ya kuwapiga chenga mabeki
kabla ya Depay kuokoa kutoka kwa mlindalango kwa kuondoa katika maeneo
ya hatari.
Kufutia ushindi huo Uholanzi wanatuchana na mshindi wa pili katika kundi A yaani Mexico.
Huku Chile ikiratbiwa kuvaana na mshindi wa kundi A yaani Brazil katika mechi za maondoano .
BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment