huu ni baadhi ya miti ambayo imepandwa katika shamba jipya lenye ukubwa wa hekali tano
hili ndilo shamba lenye miti 300 ya machenza na machungwa katika kijiji cha mkongobaki
Mzee Edward Mligo mkulima wa Matunda katika kijiji cha Mkongobaki wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe akiwa katika shamba lake la Machenza
Machenza yanayolimwa na Mzee Mligo
Shamba jipya la machenza
mzee Mligo akionesha Machenza kwa mwandishi wa mtandao huu
Wakulima wa Matunda wilayani Ludewa
katika mkoa wa Njombe wameanza kujipanga na kilimo cha mazao hayo ili
kuwauzia wawekezaji wa machimbo ya Chuma cha Liganga na Makaa ya mawe
Nkomang’ombe ambao wanatarajia kuwasili wilayani humo hivi
karibuni.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii
jana mmoja wa wakulima hao ambaye anaishi katika kijiji cha
Mkongobaki wilayani hapa mzee Edward Mligo (69) alisema kutokana na
hali inavyoonesha ya upanuzi wa barabara za maeneo ya migodi
inavyoendelea wakulima wengi wamehamasika kujiandaa kwa biashara.
Mze Mligo alisema mpaka sasa yeye
binafsi ameweza kupanda miti ya matunda aina ya Machenza na Machungwa
ipatayo 300 ambayo tayari imeshanza kuzaa matunda na ameshaandaa
shamba jingine lenye ukubwa wa hekari 5 kwaajili ya kupanda miche ya
matunda hayo ambayo imeshandaliwa.
Hata hivyo amewataka vijana kuacha
tabia ya kukaa vijiweni bila kazi badala yake wajikite katika
shughuri za uzalishaji mali ikiwemo kilimo cha matunda na ufugaji
ambao utawapa utajiri wa miaka mingi ijayo tofauti na wanavyotarajia.
“Tunaishukuru Serikali ya Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa kuikumbuka wilaya ya Ludewa kwani tumeanza
kuona dalili za kufanikisha machimbo ya madini yetu kutokana na
barabara zinazoelekea migodini kuanza kupanuliwa tofauti na awali
tulikua tukipewa maneno matupu pasipo vitendo”,Alisema Mzee.Mligo.
Hivi karibuni Serikali kupitia wakala
wa barabara nchini TANROAD wameweza kutiliana saini na makandarasi
wanne kwa gharama ya kiasi cha shilingi 7.8 bilioni ili kuzipanua
barabara za wilaya ya Ludewa na kuweka changalawe kwajili ya
upitishaji wa mitambo ya migodini.
Ukarabati wa barabara hizo umewaamsha
wakulima na wafugaji walioko wilayani Ludewa kujianda na ugeni wa
wawekezaji ambapo baadhi ya wakulima wa matunda akiwemo mzee Mligo
wamekuwa wakishinda mashambani ili kuhakikisha wanatumia fulsa ya
kilimo kujipatia kipato kwa wawekezaji hao.
Aidha wadau mbalimbali wa maendeleo
wilayi Ludewa akiwemo Huruma Mgaya wamesifu mpango wa Serikali pamoja
na Mbunge wa jimbo la Ludewa Mh.Filikunjombe kwa kazi nzuri ya ujenzi
wa barabara za lami katika mitaa ya Ludewa mjini na upanuzi wa
barabara kuu kutoka Njombe hadi Ludewa.
Bw.Mgaya alisema hali ya upanuzi wa
barabara kuu hutaharakisha maendeleo wilayani humo ingawa wananchi
walio wengi wanashauku ya kuwa na barabara ya lami itakayounganisha
wilaya ya Ludewa na ile ya Njombe kwani msimu wa mvua kiwango hicho
cha changalawe huharibika vibaya.
Aliwataka wanaludewa wanaoishi mbali
kuchangamkia fulsa za uwekezaji wilayani humo mapema kabla wageni
hawajanza kufanya mambo yao.
No comments:
Post a Comment