Mkurugenzi wa TANROAD Taifa muhandishi Mfugale ametiliana mkataba wa ujenzi wa barabara ya Itoni, Ludewa na makandarasi wanne itakayogharimu kiasi cha shilingi 7.8 bilioni ambapo ujenzi huoutatumia muda wa miezi miwili.
Akisaini mikataba hiyo Mei 12 mwaka huu katika ukumbi wa Day to Day ulioko Kibena mkoani Njombe muhandisi Mfugale alisema barabara hiyoawali itajengwa haraka kwa kiwango cha changalawe ili kuharakisha wawekezaji wa migodi ya chuma iliyoko Liganga na ile ya Makaa ya mawe Mchuhuma waweze kupitisha mitambo yao yenye uzito mkubwa.
Mhandisi Mfugale alizitanja barabra hizo kuwa ni ile ya Itoni Mlangali ambayo amepewa Boimanda modern CO.LTD,Mlangali hadi Ludewa itajengwa na Mtwivila Traders Contruction CO.LTD,Ludewa hadi Ngomang'ombe,Mchuchuma itajengwa na G;S Contractors CO.LTD NA ILE YA Mkiu hadi Liganga itajengwa Canopies International(T)LTD.
Alisema makandarasi hao watafanya kazi ya upanuzi,uvunjaji wa kona zisizotakiwa na uwekaji wa changalawe za kiwango cha juu ikiwa ni moja ya maandalizi ya ujenzi wa lami katika barabara ya Itoni,Ludewa hadi Manda.
"huu ni mwanzo tu lakini lengo kubwa la Serikali ni ujenzi wa Lami katika barabara hiyo kwani kunauchumi mkubwa sana ambao taifa linautegemea hivyo tayari kuna kampuni inaendelea na upembuzi yakinifu kwa ajili ya hiyo na tumewaagiza kila hatua wanayofikia watoe taarifa ili iingizwe katika bajeti ya mwaka 2015-2016",alisema Muhandisi Mfugale
Aidha Mbunge wa Ludewa katika Mkoa wa Njombe Deo Filikunjombe amewaonya na
kuwataka makandarasi wazarendo waliopewa na kusaini mkataba wa kazi
ya kukarabati na kupanua barabara ya Itoni hadi Ludewa kuwa waaminifu
na waadilifu vinginevyo hatasita kuomba mwongozo wa spika kwa yeyote
atakayekwenda kinyume na mkataba.
Filikunjombe alisema Makandarasi walio wengi wazarendo hawaaminiki kutokana na kufanya kazi chini ya kiwango hali inayosababisha wakose kazi wanapoomba Serikalini hivyo aliwataka kuwa mfano wa kuigwa katika ujenzi wa barabara hiyo.
Alisema ni miaka mingi hivi sasa wananchi wa wilaya ya Ludewa wamekuwa wakiahidiwa ujenzi wa barabara hiyo na uanzishwaji wa migodi ya mchuchuma na Liganga bila mafanikio lakini kwa hatua hii kwa sasa wataendelea kuwa na imani na Serikali yao.
Hata hivyo alimshukuru Rais wa Jamuhuru ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutimiza ahadi yake aliyowaahidi wananchi wa wilaya ya Ludewa ambayo ni ujenzi wa barabara na Gari ya wagonjwa.
mwisho.
No comments:
Post a Comment