Mwananchi juu ya paa la nyumba ya mtu mmoja maarufu kwa jina la Mama Mayunga, akijaribu kurusha vifuko vya mchanga katika moja ya majengo ya nyumba iliyozuka moto Jana majira ya saa 5 asubuhi mtaa wa Majengo jirani na Masangwa Guest House wilayani Misungwi mkoani Mwanza. |
Moto huo unaotajwa chanzo chake kusababishwa na jiko la gesi ulilipuka na kuiteketeza kabisa nyumba hiyo ikiwa na furniture zake. |
Huku baadhi yao wakiwa wamejitosa kufanya uokoji wa mali, wananchi wengine kama kawaida yao walikimbilia eneo la ajali kushuhudia moto huo uliokuwa ukivuma kuashiria hatari na eneo hilo si salama. |
Hali tete. |
Saa moja baadaye gari la zimamoto lilifika eneo la ajali ya moto lakini hata hivyo liliambulia kuzima magofu huku milango, madirisha na mali zilizokuwa kwenye nyumba hiyo zikiteketea kabisa. (picha na Wiliam Bundala wa matukiodaima.com kanda ya Ziwa) |
No comments:
Post a Comment