KIJANA mmoja aliyefahamika kwa jina
la Surambaya Lutemashimba (32) mkazi wa kijiji cha Maji moto
wilayani Mpanda mkoani Katavi amefikishwa katika mahakama ya wilaya Nkasi
mkoani Rukwa kujibu tuhuma zinazomkabili za kujaribu kuua.
Akisomewa mashitaka yake mbele ya
hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya Nkasi Ramadhani Rugemalila
mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi, mkaguzi msaidizi wa polisi Hamimu Gwelo
ni kuwa mtuhumiwa akiwa na wenzie watatu walimvamia mwanamke mmoja
Ng’washa Mondo (50) mkazi wa kijiji cha Mtenga wilayani Nkasi na kumkatakata
kwa mapanga kwa lengo la kutaka kuua.
Alisema mtuhumiwa huyo akiwa na
wenzie watatu baada ya kutekeleza hazma hiyo walikimbia wakiwa na imani kuwa
mwanamke huyo amekwisha kufa ambapo alizinduka baada ya kufikishwa hospitalini.
Mwendesha mashitaka huyo wa jeshi la
polisi alidai kuwa mtuhumiwa huyo sambamba na wenzake walifanya uhalifu huo
januari 7 mwaka huu nyumbani kwa mama huyo majira ya saa 2 usiku na kukamatwa
Februari 20 mwaka huu.
Alisema kuwa mtuhumiwa huyo amefanya
kosa hilo chini ya kifungu cha 211 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa
marekebisho mwaka 2002 na kuwa mtuhumiwa ana kesi ya kujibu.
Mtuhumiwa hakutakiwa kujibu lolote
baada ya mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kuisikiliza kesi hiyo ambapo kesi
itatajwa tena marchi 11 mwaka huu na kurudishwa rumande huku nje ya mahakama
wananchi walidai alichukuwa uamuzi huo kwa sababu ya wivu wa kimapenzi.
Upande wa mashitaka uliitaka
mahakama kutotoa dhamana kwa mtuhumiwa huyo kwa sababu upelelezi wa kesi hiyo
bado haujakamilika na pia watuhumiwa wengine watatu bado hawajakamatwa.
Wakati huo huo mahakama ya wilaya
Nkasi imemhukumu kwenda jela miezi sita au kulipa faini ya Tshs,40,000 Martin
Kipeta (32) mkazi wa kijiji cha Isunta wilayani Nkasi kwa kosa la
kukutwa na bangi kilogramu 300 kinyume cha sheria.
Mshitakiwa alikutwa na bangi hiyo
August 8 mwaka jana na kukutwa na kosa hilo chini ya kifungu No,12 (d) sura ya
95 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 ya sheria ya kupambana na madawa ya
kulevya.
Mtuhumiwa aliachiwa huru baada ya
kulipa faini ya Tshs,40,000 baada ya mtuhumiwa kukiri kufanya kosa hilo kinyume
cha sheria.
mwisho
No comments:
Post a Comment