Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

December 04, 2013

WANAWAKE WAONGOZA KWA MAGONJWA YA ZINAA MKOANI NJOMBE.

 Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Bwana Richard  Ngwale Akizungumza Wakati wa Maadhimisho ya sIKU ya Ukimwi Katika Kijiji Cha Itambo Kata Ya Mdandu.


 Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Bi.Esterina Kilasi Akiwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Itambo Katika Maadhimisho ya Ukimwi Akiwa Mgeni Rasmi.

 Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Shaibu Masasi Akizungumza Kwa Niaba ya Mwenyekiti wa Halmashauri Hiyo.
 Mgeni Rasmi Katika Maadhimisho ya Ukimwi Bi.Esterina Kilasi Ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Akienda Kukagua Sehemu ya Kupima Virusi vya Ukimwi.
 
Na  Gabriel  Kilamlya
 
Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Bi.Esterina Kilasi Amelaani Vikali Tabia ya Unyanyapaa n a Ukatili Unaofanywa Kwa Watoto na Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Katika Jamii.

Bi.Kilasi Amesema Kuwa Katika Wilaya ya Wanging'ombe Kumekuwa na Matukio ya Ukatili Ukiwemo Ubakaji na Kuwanyanyapaa Watu Wenye Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi Hali Inayowakatisha Tamaa ya Kuishi Watu Wenye na Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi.
Akizungumza Wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani Yaliyofanyika Katika Kijiji cha Itambo Wilayani Wanging'ombe Kwa Halmashauri za Njombe,Makambako na Wanging'ombe Yenyewe Bi.Kilasi Amesema Katika Kuadhimisha Siku ya Ukimwi ni Lazima Jamii Ikubali Kuachana na Vitendo vya Kurithi Wajane na Wagane,Kufanya Tohara Kwa Wanaume Pamoja na Kujitokeza Kuendelea Kupima Virusi Vya Ukimwi Mara Kwa Mara.

Akisoma Taarifa ya Ukimwi Katika Halmashauri ya
Njombe,Wanging'ombe na Mji Makambako Mratibu wa Ukimwi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bwana Godwin Mtui Amesema Kuwa  Mwingiliano Mkubwa wa Watu Katika Masuala ya Kibiashara,Elimu Ndogo Juu ya Ukimwi na Mila Potofu Zimezidi Kuonekana Sababu Kubwa Zinazopelekea Ongezeko la Maambukizi ya
 Ukimwi.

Aidha Amesema Kuwa Kadri Siku Zinavyokwenda Serikali Imeendelea Kukabiliana na Changamoto Hizo Ikiwemo Kuwasaidia Watumishi na Watoto Wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi.


Taarifa ya Watu Waliogunduliwa na Magonjwa ya Zinaa Imebainika Kuwa Watu 11,906 Walitibiwa Magonjwa ya Zinaa na Kati ya Hao Wanawake ni 8918 Wanaume ni 3998. 

Pamoja na Mambo Mengine Serikali Imesema Kuwa Itaendelea Kuboresha Huduma ya Dawa za Kufubaza Makali ya Virusi Vya Ukimwi Ili Waathirika hao Waendelea Kutumia Dawa Kila Siku.

Kauli Mbiu ya Siku ya Ukimwi Duniani Kwa Mwaka 2013 ni Maambukizi Mapya-Sifuri,Vifo Vitokanavyo na Ukimwi-Sifuri,Unyanyapaa -Sifuri. 


No comments: