Eneo
lililotakiwa kujengwa kumbi za maendeleo ya vijana wilayani Ludewa katika mkoa wa
Njombe limetelekezwa tokea mwaka 2003 licha ya kuwa eneo hilo
linakibao kinachoonesha kuwa kilizinduliwa na balozi wa Sweden nchini
Tanzania Mh.Sten Rylander tarehe 17/05/2003.
Uwekaji
wa kibao hicho cha uzinduzi na ujio wa balozi huyo wilayani Ludewa
uliratibiwa na shirika lisilo la kiserikali la Student Patnership
World Wide(SPW) lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea katika eneo
hilo lililopo Ludewa mjini na kusababisha kuwepo msitu.
Kwa
mujibu wa maelezo ya mashuhuda katika uzinduzi wa kibao cha ujenzi wa
eneo hilo ambao hawakutaka kutajwa majina yao walisema malengo ya
ujenzi yalikuwa ni kujenga kumbi tatu kwaajili ya vijana ili
kupunguza maambukizi ya virus vya ukimwi.
Walifafanua
kuwa mpaka sasa hakuna kinachoendelea kwani pamekuwa ni vichaka
ambavyo ni vificho vya waharifu na bado haijulikani fedha za ujenzi
wa kumbi hizo ambazo zilidhaminiwa na Ubalozi wa Sweden kama zimeliwa
au zilihifadhiwa.
Alipotakiwa
kulitolea maelezo suala hilo mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Solomon
Madaha alisema hana taarifa na ujenzi wa kumbi hizo hivyo
atalifuatilia na kujua kulikoni na kwanini mpaka sasa kumbi hizo
hazijajengwa eneo hilo.
“Sina
taarifa sahihi ya ujenzi wa kumbi hizo kwani ni inaonesha ni kipindi
kirefu kimepita mpaka sasa na hakuna aliyestukia kama kunakibao
kilichozinduliwa na Balozi wa Sweden kule vichakani,hivyo
nitalifanyia kazi suala hili”,alisema Bw.Madaha.
Bw.Madaha
alisema ni jambo jema kama shirika hilo la SPW lilipewa kazi ya
kusimamia ujenzi wa kumbi hizo na ubalozi wa Sweden kani vijana wa
wilaya ya Ludewa hawana kumbi za kukutania na kujadili mambo yao hasa
kufanya mazoenzi ya sanaa mbalimbali.
Aidha
viongozi wa shirika hilo walipotafutwa kwa njia ya simu
hawakupatikana lakini bado juhudi za kuwatafuta ili waweze kutolea
maelezo yanayohusu ujenzi wa kumbi hizo zinaendelea ingawa kuna tetesi
kuwa shirika hilo limebadiri jina na ofisi zao ziko mkoani Iringa.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment