Waandishi wa habari wameaswa
kufuata maadili ya taaluma yao
ili kutoviingiza vyombo vya habari katika matatizo na kuipotosha jamii.
Wito huo umetolewa jana na
M/kiti wa halmashauri ya wilaya ya makete Mh.Daniel Okoka aliyekuwa mgeni rasmi
wakati akifungua mafunzo ya kuijengea uwezo bodi ya redio kitulo fm pamoja na
wakuu wa Idara kwa ufadhili wa mfuko wa kusaidia vyombo vya habari nchini
Tanzania Media Fund(TMF) mafunzo hayo yatakayochukua siku 5 kuanzia jana hadi
ijumaa ya tarehe 21 disemba mwaka huu
Ktk mafunzo hayo
yalihodhuriwa na wanahabari kutoka kitulo fm redio,bodi ya redio na muwezeshaji
Dr.Alfred Rwechengula ktk kuhakikisha redio inaingiza kiasi kikubwa cha mapato kwa njia ya uboreshaji wa vipindi
vyenye kuelimisha jamii
Jumla ya wanahabari 10
wameanza kupata mafunzo hayo ili kuelimisha jamii ya wanamakete na nje ya
makete pia ili kuongeza uelewa kwa wanajamii hasa katika Nyanja za
Elimu,Afya,Mazingira pamoja na Biashara
Redio kitulo fm ambayo
ilianzishwa mwaka 2005 kwa msaada wa UNICEF kwa kushirikiana na Halmashauri ya
wilaya ya Makete
Mh.Okoka ametaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kuwa ni
pamoja na wananchi kupata habari za Makete na duniani kwa ujumla kwa wakati
muafaka,kuwahamasisha vijana kujishughulisha na maendeleo ktk jamii,imetoa
ajira kwa vijana wenye taaluma ya uandishi wa habari na Utangazaji,imesaidia
kutangaza matangazo ya halmashauri na kuwafikia walengwa kwa wakati
Hata hivyo amezitaja baadhi
ya changamoto ambazo redio inakumbana nazo kuwa ni pamoja na vifaa duni hivyo
kutofikia baadhi ya maeneo hata katika wilaya ya makete,kituo kinaingiza mapato
kidogo pamoja na kuwa na idadi ndogo ya wanahabari waliopo kituoni hapa.
No comments:
Post a Comment