Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiongea wakati wa mazishi Baba wa Demokrasia wa
Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kijijni Qunu, Eastern Cape, Afrika
Kusini leo Desemba 15, 2013.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa
Afrika (AU) Dkt Dlamini Zuma kwa hotuba ya kusisimua aliyoitoa wakati
wa mazishi Baba wa Demokrasia wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela
kijijni Qunu, Eastern Cape, Afrika Kusini leo Desemba 15, 2013. Kushoto
ni Mwenyekiti wa SADC na Rais wa Malawi Mhe. Joyce Banda. Rais Kikwete
alialikwa kuzungumzia sifa za mapambano ya ukombozi aliyoongoza Mzee
Madiba ambapo Tanzania ndiyo ilikuwa ni nchi yake ya kwanza kusaidia
mapambano yote ya ukombozi kusini mwa Afrika kwa kuwahifadhi na kuwapa
misaada ya hali na mali wapigania ukombozi wake.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na wageni wengine akitoka katika hema
maalumu lililotumika kwa shughuli za mazishi Baba wa Demokrasia wa
Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kijijni Qunu, Eastern Cape, Afrika
Kusini leo Desemba 15, 2013. Wa tatu kulia ni Mrithi wa kiti cha Ufalme
wa Uingereza Prince Charles.
PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment