WANANCHI
wa kijiji cha Amani Wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe wamegoma
kupokea taarifa ya mapato na matumizi ya mwaka huu na kuitaka
serikali ya kijiji hicho kusoma kwanza taarifa ya mapato na matumizi
ya miaka mitano iliyopita ili kuondoa hofu na mashaka juu ya tuhuma
za ubadhirifu wa fedha na mali zinazowakabili viongozi wa kijiji
hicho.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wananchi wa kijiji cha Amani kinachoongoza kwa
kuwa na utajiri wa madini ya dhahabu wilayani Ludewa wamesema
hawajawahi kusomewa taarifa ya mapato na matumizi zaidi ya miaka
mitano hali ambayo imeanza kuwatia hofu na kutokuwa na imani na
uongozi wao.
Kwa
upande wake Joseph Mlelwa ambaye ni mkazi wa kijiji cha Amani
alisema ni miaka zaidi ya mitano Serikali ya kijiji hicho inaendelea
kuwahimiza kushiriki katika shughulu za maendeleo huku wakichangishwa
michango mbalimbali lakini hawajui fedha zao zinafanyakazi gani na
wala hawana taarifa juu thamani ya nguvu wanazoendelea kuchangia.
“”””kijiji
hicho kina miradi mingi ya maendeleo ikiwemo machimbo ya madini aina
ya dhahabu,ufugaji,vitaru vya kahawa,Power tiller,Trector na miradi
ya ujenzi wa shule ya Sekondari lakini wananchi hawajapata
kufahamishwa nini kinaendelea na miradi hiyo imezalisha kitu gani kwa
muda mrefu sasa bado tuko gizani katika taarifa ya mapato na matumizi
ya kijiji chetu.’’’’’’ alisema Mlelwa
Mlelwa
akaongeza kuwa kila kukicha wamekuwa wakishuhudia kubadirishwa kwa
maafisa watendaji wa kijiji na si kutoa taarifa ya mapato na matumizi
ya kijiji kwa wananchi hali ambayo inawakatisha tamaa wananchi
kuendelea kufanya kazi za maendeleo hasa katika shule yao ya kata
kama ilivyo maeneo mengine.
“’’’’
tunashangazwa
na hali inayotokea kijijini hapa tofauti na vijiji vingine wilayani
Ludewa na kijiji hiki ndicho chenye machimbo ya Dhahabu lakini hakuna
taarifa zozote za mapato na matumizi licha ya kuwa kijiji hiki kina
miradi mingi tofauti na vijiji vingine na hakuna kiongozi yeyote
anayeona umuhimu wa jambo hili.’’’’” walilalamika baadhi ya
wananchi ambao hawakupenda majina yao yaanikwe.
Waliongeza
kuwa mikutano ya hadhara ya kijiji hufanyika na baadhi ya taarifa
nyingine hutolewa lakini ikifika muda wa kusoma taarifa ya mapato na
matumizi viongozi hao hudai muda hautoshi hivyo taarifa hiyo
huahirishwa kila mwaka na hofu ya wananchi ni kwamba kuna uwezekano
mkubwa wa harufu na kila dalili za ufisadi.
Afisa
Mtendaji wa kijiji cha Amani Atanas Mwalongo alikiri kuwepo kwa
tatizo hilo na kusema kuwa ni miaka mitano hivi sasa imepita wananchi
wahajaweza kusomewa taarifa ya mapato na matumizi na sababu kubwa
bado hazija eleweka kutokana na uongozi uliopita kuhamishwa na
wengine kuacha kazi.
‘’’’ tangu
nihamie katika kijiji cha Amani ni takribani mwaka mmoja na nusu
nimeweza kufanya kazi kijijini hapa lakini kila nikitaka kutoa
taarifa yangu kwa kipindi nilichokuwepo wananchi hukataa na kutaka
zisomwe taarifa za miaka mitano ya nyuma wakati yeye hahusiki na
taarifa hizo kutokana na aliyekuwa mtendaji wa kijiji hicho kuhamia
kijiji cha Mfarasi.’’’’’ alilalamika Mwalongo
Mwalongo
akaongeza kuwa amejaribu kufanya mawasiliano na Afisa mtendaji
aliyempokea Oktavian Mtewele aliye hamia kijiji cha Mfarasi bila
mafanikio hivyo bado anaendelea kufuatilia taarifa za awali ili
kumaliza mgogoro kwa wananchi ambao ni haki yao kufahamishwa mapato
na matumizi ya kijiji chao.
Kwa
mujibu wa wananchi kijiji hicho kina miradi mingi ya maendeleo na
hivi sasa kuna baadhi ya madarasa yanakarabatiwa ili yaweze
kufunguliwa na mbio za mwenge wa Uhuru hivyo wananchi wanapaswa
kushikamana katika kuhakikisha kazi za maendeleo zinatekelezeka na si
kususia.
No comments:
Post a Comment