Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

September 20, 2013

AFISA MTENDAJI ASOMEWA MAKOSA 14 YA RUSHWA ,ALIWAPA WAKULIMA FEDHA BADALA YA PEMBEJEO.





WATU watatu, Daudi Luoga, wakala wa pembejeo, Rashidi Mlelwa ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya pembejeo na Tito Haule ambaye ni afisa mtendaji wa kijiji cha Mavanga wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe wamefikishwa mahakamani kwa makosa 14 ya rushwa.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya hakimu mkazi mfawidhi katika mahakama ya wilaya ya Ludewa Fredrick Lukuna mwendesha mashtaka wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini Richardi Marekano alisema washtakiwa wote kwa pamoja walitenda makosa hayo katika mwaka wa kilimo wa mwaka 2011/2012.

Marekano akaiambia mahakama hiyo kuwa washtakiwa walitenda makosa hayo chini ya kifungu cha 15 1(A) na kuonngeza kuwa washtakiwa waliwashawishi wakulima kutia saini katika vocha za pembejeo na kuwalipa fedha kati ya shilingi 20,000 na 30,000 wakidai kuwa ni kifuta jasho kwao kutokana na serikali kuleta pembejeo kwa kuchelewa.

Washtakiwa walikana mashtaka yanayowakabili na kutekeleza masharti ya dhamana na kuachiwa hadi oktoba 18 mwaka huu kesi itakapokuja kwa kusikilizwa kwa hatua ya awali.

Aidha katika mahakama hiyo mganga wa hospitali teule ya wilaya ya Kilolo(Ilula) katika mkoa wa IringaDaktari Adamson Ndapisi amefikishwa katika mahakamani ya Hakimu mkazi kwa makosa tisa ikiwemo kugushi barua na saini za watumishi wenzake na kujipatia jumla ya shilingi m.3.3 mali ya serikali.

Mbele ya hakimu mkazi mfawidhi katika mahakama ya wilaya ya Ludewa Fredrick Lukuna mwendesha mashtaka wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Njombe Richard Marekani akaiambia mahakama kuwa mshtakiwa Adamson Ndapisi alitenda makosa hayo aprili 2008 akiwa mratibu wa bima ya afya wilaya.

Katika shtaka la kwanza Marekano akaiambia mahakama kuwa mshtakiwa aligushi barua ya kuomba shilingi m.3.3 katika Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kwa lengo la kuendesha semina hewa kwa watumishi wa idara ya Afya huku akijua ni uongo chini ya kifungu 333, 335,(d) 1 kanuni ya adhabu sura ya 16.

Makosa mengine ni matumizi mabaya ya madaraka chini ya kifungu 22 kanuni ya adhabu ya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2002 ambapo mshtakiwa anatajwa kughushi risiti yenye thamani ya jumla ya shilingi milioni 2.1 na kuwasainisha watumishi wa idara ya afya huku akitambua kuwa ni kosa.

Aidha mfanyabiashara maarufu wa mgahawa wa NAM CAFE ulioko mjini Ludewa Maria Haule(Mama Neema) ambaye katika kesi hiyo ni mshtakiwa wa pili yeye anakabiliwa na kosa moja la kushiriki kuidanganya serikali kwa kutoa risiti za vyakula hewa zinazoonesha kuwa mshtakiwa alinunua vitu dukani kwake kosa linaloangukia katika fungu la namba 30 ya sheria ya kuzuai na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Washtakiwa wote walikana kuhusika na makosa yanayowakabili, na kudhaminiwa hadi Oktoba 18 mwaka huu kesi itakapokuja kwa kutajwa tena.


mwisho

habari hii ni kwa udhamini wa Lukotiko bucher.

Ni wauzaji wa nyama ya Ng'ombe wa kienyeji wanapatikana wilayani Ludewa.
ufikapo wilayani Ludewa wanapatikana sokoni katika jengo la soko la Samaki.

kwa nyama bora kwaajili ya harusi,sherehe na misiba onana na Lukotiko bucher. 
 pia tunanunua ng'ombe wa kienyeji katika vijiji vyote wilayani Ludewa.

kwa mawasiliano zaidi tupigie simu namba 0765878297/0764096248/0765796655 na 0755194056.
kutana na Lukotiko Bucher kwa nyama bora.

 

No comments: