Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

July 19, 2013

TAKUKURU WAANDAA MASHINDANO YA POOL LUDEWA.


Washindi wa kwanza katika mchezo wa pool wakikabidhiwa zawdi yao kutoka kwa kamanda wa TAKUKURU Bw.Mwakambonja



 Mmiriki wa Leaders Club iliyoko wilayani Ludewa Mhandisi.Mkuya akisoma matokeo ya washindi
Mwamuzi wa pambano hilo akipokea zawadi







TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe imeandaa mashindao ya pool yaliyowashirikisha wadau mbalimbali wilayani huo ili kuinua vipaji vya wachezaji wa mchezo huo.

Mashindano hayo yalifanyika katika Baa ya Leaders Club iliyoko wilayani hapa ambapo uliibuka mpambano mkali kati ya timu tatu baada ya timu nyingine kutolewa ndipo alipoweza kupatikana mshindi aliyejinyakulia kitita cha shilingi 60000 na kufuatiwa na mshindi wa pili ambaye alipata shilingi 45000 na watatu alipata 30000.

Akitoa zawadi kwa washindi Kamanda wa TAKUKURU wilayani Ludewa Bw.Edings Mwakambonja alisema mashindao hayo ni mwanzo tu lakini ofisi yake inampango wa kufanya mashindano ya michezo mbalimbali ili kuinua vipaji na kuwasogeza wananchi katika elimu dhidi ya rushwa.

Bw.Mwakambonja alisisitiza kuwa na ushirikiano miongoni mwa jamii katika kufichua mambo maovu ili kuliweka Taifa katika hali ya amani kwani rushwa ni adui wa haki hivyo kama kila mwananchi atatambua wajibu wake rushwa itakoma.

Nimefurahishwa na mashindao haya jinsi yalivyopata upinzani baina ya wachezaji lakini niwaahidi ofisi yangu haitaishia hapa hata wewe uliyeshindwa safari hii jipange ili mashindano yajayo uweze kuibuka na ushindilakini bila kusahau kupiga vita rushwa”,alisema Bw.Mwakambonja.

Aidha mmiliki wa baa ya Leaders Club Mhandisi Baraka Mkuya aliisifu TAKUKURU kwa kuanzisha mashindano hayo kwani mara nyingi yeye ndiye amekuwa akidhamini mashindano hayo.

Mhandisi.Mkuya aliyema kama TAKUKURU watakuwa wakishirikiana na jamii katika kudhamini michezo mbalimbali na kutoa elimu dhidi ya Rushwa basi anaamini jamii itakuwa na uelewa mpana wa kupinga na kuvitolea taarifa vitendo vyote vta rushwa wilayani humo.

Aliyema maeneo ya baa ndipo mara nyingi watu hupeana rushwa hivyo kwa kutoa elimu ya udhibiti wa rushwa katika baa ndiyo sehemu muafaka na kila raia natakuwa macho kumwangalia mwenzake nini anakifanya.

Mhandisi.Mkuya alizitaka mamlaka nyingine yakiwemi makampuni ya vinywaji kutoisahau wilaya ya Ludewa katika kudhamini michezo mbalimbali ukiwemo mchezo wa pool kwani wilaya hiyo imekuwa ikisahaulika na wadhamini kwa muda mrefu sasa.

Mwisho.

No comments: