Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

July 01, 2013

OBAMA AWASILI TANZANIA



Obama akiwa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete

Rais wa Marekani Barack Obama amewasili nchini Tanzania leo Jumatatu kwa zara ya siku mbili, ikiwa ni kituo chake cha mwisho cha ziara yake barani Afrika akitokea nchini Afrika Kusini.

Obama ambaye ameambatana na mkewe Michelle Obama amepokelewa na mwenyeji wake rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Salma Kikwete katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na kisha kuelekea Ikulu ya rais.




No comments: