Bank ya NMB tawi la
wilaya ya Ludewa katika mkoa wa Njombe imewataka wateja wa benk wilayani humo
kuwa na siri ya taarifa zao ili kuepusha wizi wa fedha unaoweza kuwakumba
wateja hao.
Akiongea na waandishi wa
habari jana meneja wa bank ya NMB lawi la Ludewa Bw.Maulid Abdalah Mwingira
alisema kumekuwa na wateja ambao hawana siri juu ya taarifa zao za kibenk hali
ambayo inasababisha wateja hao kuibiwa fedha zao na kuilaumu bank wakati kosa
liko kwa wateja hao.
Alisema baadhi ya wateja
wamekuwa wakiwaamini sana watoto na jamaa na marafiki zao na kuwapatia namba za
siri za account zao na baadae kuibiwa fedha bila kujitambua na kupelekea
kuilaumu bank bila msingi wowote.
“napenda kuweleza wateja
wetu kuwa wasipende kutoa taarifa zao za kibenk kwa kila mtu kwani wanaweza
kuibiwa fedha zao na watu wanaowaamini,na watambue kuwa kupitia mitandao ya
simu mtu anaweza kuhamisha fedha kutokana na wewe kumpa taarifa zao za
kibenk”,alisema Bw.Mwingira.
Bw.Mwingira alisema Bank
hiyo ina wateja wengi sana nchini na kama kila mteja atakuwa na tabia ya
kutunza taarifa zake vizuri basi hakuna mtu mwingine atakayeweza kuiba fedha
katika account ya mwingine lakini kama mteja mwenyewe hatakuwa na siri katika
taarifa zake basi ataruhusu kuingiliwa.
Aidha aliwataka
wanaoibiwa kwa uzembe wao wenyewe wasiwe na kauli ya kuichafua bank hiyo kwani
wafanyakazi wa bank ya NMB Tanzania ni waadirifu na wako makini na kazi
wanazozifanya na si vinginevyo
Kuhusiana na Mitandao ya
simu kuathiri huduma za kibenk Bw.Mwingira alisema hakuna athari yoyote ya
mitandao hiyo katika shughuri za kibenk kutokana na mahusiano mazuri ya
mitandao hiyo na Bank.
Alisema kupitia mitandao
ya simu wateja wa bank wanaweza kuweka na kutoa fedha bila ya kufika bank hali
ambayo imewarahisishia wafanyakazi wa bank kutokuwa na mzigo mkubwa na kuweza
kukusanya marejesho ya mikopo kwa kutumia mitandao hiyo.
Bw.Mwingira alisema kila
kitu kina faida na hasara ndivyo ilivyo mitandao ya simu katika huduma za
kibenk kwani kuna watu ambao pia hutumia mitandao hiyo katika wizi wa fedha
nchini kwa baadhi ya bank.
Hali ambayo inawafanya
wafanyakazi wa bank kuwa makini na kazi yao na katika kufuatilia account zote
ili kubaini kama kuna wizi unaoweza kujitokeza kwa kutumia mitandao hiyo na
waliobainika kutumia vibaya mitandao ya simu wameshachukuliwa hatua za kisheria
ili kukomesha wimbi la wizi wa mitandao.
Bw.Mwingira aliwataka
wateja kuwa waangarifu na taarifa zao pia kuuliza kwa wafanyakazi wa bank hiyo
pale wanapoona kunautata ama hawajaelewa na si kulaumu kwa vitu
wasivyovifahamu,ili kupata ufumbuzi mapema iwezekanavyo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment