Mazingira ya Shule ya Sekondari Ludewa ambayo ni shule ya wazazi inayomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi(CCM)
Baadhi ya majengo ya shule ya Sekondari ya Ludewa
Dada mkuu wa shule hiyoCraudia Nkwera na Kaka mkuu Joel Kayombo
Wazazi
wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wametakiwa kutoa ushirikiano kwa walimu
wa shule za Sekondari na Msingi ili kuleta ufanisi wa elimu kwani kushuka kwa
elimu kunatokana na wazazi hao kutofuatilia maendeleo ya watoto wao.
Hayo
yalisemwa na mwalimu mkuu Paulo Matunduru wa shule ya sekondari Ludewa shule ya
wazazi ambayo inamilikiwa na chama cha mapinduzi wakati akiongea na waandishi
wa habari walipokwenda kumtembelea katika shule yake.
Mwalimu
Matunduru alisema,wazazi wengi hawafuatilii maendeleo ya watoto wao pindi
watokapo shule hali ambayo inawafanya wanafunzi walio wengi kujisahau na kuwa
wazembe madarasi kielimu.
Alisema kama
walimu na wazazi watashirikiana kikamilifu katika kufuatilia maendeleo ya
wanafunzi basi tatizo la kufeli katika mitihani litapungua kwa kiasi kikubwa
nchini na malalamiko ya wadau wa elimu hayatakuwepo.
“kama wazazi
watashirikiana na walimu katika kufuatilia maendeleo ya wanafunzi kuanzia shule
za msingi na zile za sekondari kwa kukagua daftari na mitiahani wanaporudi
majumbani hali ya elimu nchini itakua na hata kiwango cha ufaulu katika
mitiahani kitaongezeka”,alisema Mwalimu Matunduru.
Alisema
imefikia wakati baadhi ya wazazi wamesahau wajibu zao kwa kuwatelekeza watoto
mashuleni na kutofuatilia maendeleo yao hali ambayo inasababisha wanafunzi
wengi kufanya vibaya kutokana na kukosa ufuatiliaji.
Aidha
alizitaja changamoto zinazo ikumba shule hiyo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa
bwalo la chakula kwani mpaka sasa uongozi wa shule umelazimika kutenga chumba
kimoja cha darasa kutumika kwaajili ya chakula.
Alisema
shule hiyo inampango wa kuanzisha masomo ya kidato cha tano na cha sita lakini
bado majengo yake yanahiotaji ukarabati mkubwa ikiwemo ujenzi wa bwalo la
chakula ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi.
Changamoto
nyingine inayoikabili shule hiyo ni pamoja na ubovu wa barabara ya kuingia
shuleni hapo kwa baadhi ya gari zinashindwa kuingia kutokana na barabara ya
awali kuharibika vibaya na mvua.
Mwalimu
Matunduru aliwaomba wahusika wakuu wa shule hiyo kusaidia kukabili changamoto
hizo kwani ni shule kongwe wilayani hapa hivyo haipaswi kusahaulika kiasi hicho
ikizingatiwa im ezalisha wasomi wengi wanaofanya kazi katika kada mbalimbali
Serikalini na binafsi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment