katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Taifa Nape Nnauye akisalimiana na wananchi wa wilaya ya Ludewa
Kinana akiongea na wananchi wa kata ya Ludewa mjini
Wananchi wakimsikiliza mbunge wao Deo Filikunjombe hayupo pichani
Wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara
Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi
Taifa Bw.Abdulrahman Kinana jana aliwahakikishia
wananchi wa wilaya ya Ludewa katika Mkoa wa Njombe kuwa viwanda vya uzalishaji
wa chuma na makaa yamawe vitajengwa wilayani humo na si kwingineko.
Kauli hiyo ya Kinana imekuja baada ya
kuvuma tetesi kuwa viwanda hivyo kunauwezekano mkubwa wa kujengwa Bagamoyo
hivyo wananchi wa wilaya ya Ludewa walikuwa na shauku ya kujua ujemzi wa
viwanda hivyo.
Alisema kutokana na ukubwa wa miradi
hiyo miwili ambayo inatarajia kuanza miaka ya 2015 na 2016 na kubadiri taswira
nzima ya wilaya ya Ludewa haitaweza kujengwa eneo jingine zaizi ya wilaya hiyo
na kusambaza umeme huo nchi nzima.
Bw. Kinana aliwataka wananchi wa wilaya
hiyo kuwa makini na watu wanaoeneza habari za uwongo ambazo zinalengo la
kujenga chuki miongoni mwa jamii na viongozi kwani kinachotakiwa zaidi ni
kuisikiliza Serikali kupitia kwa Mbunge wa jimbo hilo.
“Tumekuwa tukifanya kazi vizuri na Mbunge
wenu Filikunjombe hivyo kinachotakiwa kumsikiliza na kumuamini kwani chochote
anachowaeleza kinatoka Serikalini na si vinginevyo hata hao wanowadanganya
kuhusiana na ujenzi wa viwanda wakataeni”,alisema Bw.Kinana.
Alisema Serikali ya CCM inafurahishwa na
utendaji wa Mh.Deo Filikunjombe kwani ni mfano kwa wabunge wengine wa chama
hicho kutokana na kujiamini katika kutetea wananchi wake awapo Bungeni.
Katika hatua nyingine Wananchi
wa jimbo hilo walionyesha kumbana kiongozi huyo
kwa kuhoji sababu ya wabunge wa CCM bungeni kufanya
kazi ya kukipongeza chama chao huku wengi wao
wakiwa kimya (mabubu) katika kuchangia na wale wanaochangia
kama mbunge wao Filikunjombe wamekuwa waklichukiwa kuwa
ni wapinzani ndani ya CCM .
Hivyo wananchi hao
kumweleza katibu mkuu huyo aliyeongozana na katibu wa itikadi na
uenezi wa CCM Taifa Nape Nnauye kuwa wao
wataendelea kumuunga mkono mbunge Filikunjombe kwa vipindi
vingine tena vitatu vya miaka 15 hadi mbunge mwenyewe
atakapoamua kuacha kugombea na iwapo watafanya mchezo basi
wao watamfuata mbunge huyo kokote atakakokuwa.
" Mheshimiwa
tunaomba leo chama kitueleze hivi kwanini wabunge wa CCM
wamekuwa si msaada kwa wapiga kura wao muda wote
wamekuwa kimya bungeni na wale wanaochangia wanachangia
kupongeza chama, tunaomba kukueleza kuwa sisi
tupo na mbunge wetu na hata wana CCM wanaojipitisha
jimbo la Ludewa wakiamini sisi tutayumba uwaeleze kuwa
CCM hatudanganyiki "alihoji mwananchi aliyejulikana kwa jina la
Optatus Kalungu.
Akizungumza jana na
wananchi wa wilaya ya Ludewa ambao walikusanyika kwa
wingi katika mkutano wa hadhara kwa lengo la kutaka kusikia
kauli ya CCM juu ya uamuzi utakaochukuliwa kwa mbunge wao
kutokana na kuwepo kwa kauli za chini kwa chini katika jimbo hilo
kuwa ziara ya Kinana jimboni humo ni kutaka kumshughulikia mbunge
huyo.
Hata hivyo Kinana aliwataka
wananchi wanaounga mkono uamuzi wa kuendelea kumwongezea muda wa
vipindi vitatu Filikunjombe kunyosha mikono juu na
baada ya wananchi wote kunyosha mikono yao juu
alisema pia kwa upande wake anaungana na wao na kuwa chama hakitafanya
makosa kwa kuwasaliti kuwapa mtu mwingine katika uchaguzi
ujao wa mwaka 2015 .
"Hata mimi katibu
mkuu naungana na uamuzi wenu wa kumwongeza muda Filikunjombe na
napenda kuwahakikishia kuwa CCM haitafanya makosa
itaendelea kuwaachia Filikunjombe kama mlivyomchagua wenyewe labda
ashindwe yeye " alisema Kinana.
Kwa upande wake
Filikunjombe alisema mbali ya kuanza mradi mkubwa wa lami katika
wilaya hiyo wa kuanzani Itoni Njombe hadi Manda ila bado kuna mradi
wa maji wenye thamani ya Tsh bilioni 1.5 ambao utaondoa adha ya maji
katika mji wa Ludewa ambayo ndio kero kubwa kwa wananchi wake.
Filikunjombe alisema katika
mji wa Ludewa tayari Serikali imetenga fedha za kutengeneza barabara za mitaa
kwa kiwango cha lami kilometa kumi na ujenzi huo unaanza mara moja hivi punde
hivyo wananchi wanatakiwa kutoa ushirikiano kwa kampuni iliyopewa tanda hiyo.
Alisema kutokana na kuendelea
kuutamani ubunge wake ataendelea kuwatumikia vema wananchi na
kamwe siku zote hatarudi nyuma bungeni katika kuwapigania
wananchi hao
Mwisho.
No comments:
Post a Comment