Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

May 27, 2013

KATIBU MKUU WA CCM TAIFA ABDULRHMAN KINANA NA NAPE WAINGIA MKOANI NJOMBE.



Kinana akisaini kitabu cha wageni Uwanja wa Ndege wa Iringa baada ya kuwasili uwanjani hapo asubuhi jana. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Joyce Msavatavangu


Nape akisaini kitabu cha wageni
 



Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakisalimia baadhi ya viongozi, baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Iringa asubuhi jana, kwa ajili ya kuanza ziara ya siku saba, mkoani Njombe. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Joyce Msambatavangu.
 



Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  akiwa na viongozi wa mkoa wa Iringa. Nyuma ni Nape Nape naye akiwa na wenyeji.
 


Katibu Mkuu wa CCM Taifa Mhe.Kinana afanya mazungumzo na Wakazi wa Iringa Mapema jana kabla ya kuanza safari ya Siku sita Mkoani Njombe kuanzia leo may 27 

Katika hatua Nyingine Katibu Kinana na Katibu Mwenezi wa CCM Taifa Nape Mnauye watafanya kazi ya kuzindua tawi la Chama katika Eneo la Mizani MAKAMBAKO Mkoani Njombe pamoja na Kuzungukia Wilaya zote za Mkoa wa Njombe.

Aidha Katibu Kinana atawasili Wilayani Makete May 30 mwaka Huu na Julai Mosi mwaka Huu atakuwa Wilaya ya Wanging'ombe. 

Majira ya Alasiri Kinana atawasili Mkoani Njombe na Msafara wake tayari kwa Ziara ya Siku sita Mkoani Njombe.

Kesho May 28 mwaka huu  katibu huyo pamoja na Msafara wake atakuwa Wilayani Ludewa na May 29 atakuwa Wilayani Njombe kabla ya Kuwasili Wilayani Makete may 3o mwaka Huu.

Kwa Mujibu wa Taarifa za Ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe Kupitia katibu wake Mkoa bwana Hosea Mpagike,Kinana atafanya ziara na Kuondoka Juni Mosi Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe. 


Na Gabriel Kilamlya,Njombe. 



No comments: