.
kibao cha jiwe la msingi ambacho kiliwekwa na Bi.Monica Mchilo ambaye ni Diwani wa kata ya Ludewa kwa niaba ya Mbunge wa jimbo la Ludewa Bw.Deo Filikunjombe
Katibu wa mradi wa ukamuaji wa mafuta ya alizeti Bw.Joseph Mvanga akisoma taarifa ya mradi huo siku ya uzinduzi wa jengo hilo
Jengo la mashine za ukamuaji wa mafuta ya alizeti likiwa bado halijakamilika
Mh.Monica Mchilo akiwa na padre.Geofrey Mtulo katika uzinduzi wa jengo hilo
waumini wa kanisa la anglikana la Ludewa mjini wakiandamana kuelekea katika jengo la mashine za ukamuaji wa mafuta ya alizeti
Mh.Mchilo akikata utepe kuzindua jengo hilo
Mvanga akitoa maelezo kuhusiana na ujenzi wa jengo hilo mbele ya diwani wa kata ya Ludewa Bi.Monica Mchilo
Bi.Monica Mchilo akiwa na padre.Geofrey Mtulo katika jengo hilo
Waumini wakishuhudia uzinduzi huo
Baadhi ya mashine zikiwa bado hazijafungwa katika jengo hilo.
Mbunge wa jimbo la Ludewa katika mkoa wa NjombeBw.Deo Filikunjombe jana aliweka jiwe la msingi katika jengo la mashine za kukamua mafuta ya alizeti katika Kanisa la Watakatifu wote mtaa wa Ludewa mjini ambapo juhudi za mradi huo zimetokana na nguvu za waamini wa kanisa hilo.
Akitoa taarifa za ujenzi wa mradi huo katibu wa kanisa la Anglikana la Ludewa mjini Bw.Joseph Mvanga alisema mradi huo wa mashine za kukamua mafuta ya alizeti ulibuniwa na waumini Desemba 2011ukiwa na lengo la kuinua kipato cha waumini hao badala ya kutegemea michango na sadaka.
Hivyo mikakati ya upatikanaji wa mashine hizo ulianza kupitia michango ya hali na mali kutoka kwa waumini wa kanisa hilo na makanisa mengine ya jirani,wahisani mbalimbali na harambee ambapo wadau walishiriki na hatimaye zikapatikana jumla ya shilingi milioni 7.
Bw.Mvanga alisema ilipofika tarehe 5 Augast 2012 wazo la ununuzi wa mashine hizo lilikamilika la kupata mashine ya kukamua mafuta ya alizeti yenye thamani shilingi milioni 5.5 hiyo ilikuwa ni gharama ya ununuzi wa mashine na usafirishaji wa mashine hizo kutoka jijini Dar es salaam hadi wilayani Ludewa.
Mashine hizo zitakazofanya kazi katika kata ya Ludewa zitakuwa ni ukombozi kata za jirani zaidi ya kata saba ambapo kwa muda mrefu sasa wananchi wamekuwa wakilima zao la alizeti bila kuwa na soko la uhakika kupitia mradi huo hakuna mwananchi atakayeshindwa kunufaika kama maeneo mengine.
“tunawashukuru wadau mbalimbali walioweza kutumia nguvu zao na michango ya hali na mali katika kufanikisha ununuzi wa mashine hizi kwani kwetu sisi waumini wa kanisa la Anglikana na dini nyingine tumepata ukombozi hivyo wasichoke kushirikiana nasi katika kuendeleza mradi huu”,alisema Bw.Mvanga.
Bw.Mvanga alisema ujenzi wa jengo hilo la mashine umefikia pahala pazuri kwani kilichojengwa ni kuta za jengo hilo la tayari limeshaezekwa bati ambapo thamani ya shilingi milioni 7.2 zimetumika kati ya hizo nguvu kazi za waumini ni shilingi million 1 na fedha taslimu ni shilingi 6.2 milioni.
Alisema kazi zilizobaki katika kukamilisha ujenzi wa jengo hilo ni upigaji lipu na sakafu,fremu na shata za milango na madirisha,dari na rangi,ambapo jumla ya shilingi milioni 4.5 zinahitajika ili kukamilisha jengo hilo vinyo mpaka jengo hilo linakamilika litatumia shilingi milioni 17.2.
Akiweka jiwe la msingi katika jengo hilo la mashine za kukamua mafuta ya laizeti kwa niaba ya mbunge wa jimbo la Ludewa Diwani wa kata ya Ludewa Bi.Monica Mchilo aliwapongeza waumini hao kwa michango yao iliyopelekea kufanikisha mradi huo.
Bi.Mchilo alisema ni mfano wa kuigwa kwa taasisi mbalimbali kwani maisha bora kwa kila mtanzania hayaji bila ubunifu kwa hatua hiyo ni matarajio makubwa ya kuwa na mashine nyingine zikiwemo za usindikaji wa unga ili kwenda sambamba na ushindani wa kibiashara hasa kwa wawekezaji wanaotarajia kufanya kazi wilayani Ludewa.
Alisema jamii inapaswa kutambua watakao nufaika na mradi huo si waumini wa kanisa hilo pekee bali ni raia wote wanaoishi wilaya ya Ludewa na nje ya Ludewa hivyo atashirikiana nao kuona mradi huo unafanikiwa kama ulivyokusudiwa.
Aidha Padre wa kanisa hilo Geofrey Mtulo alimshukuru Bw.Filikunjombe kwa kuwaunga mkono kwa kumtuma mwakilishi katika uzinduzi wa jengo hilo kwani waumini wamepata faraja kwa tukio hilo.
Padre Mtulo aliwataka waumini kuendelea kuwa na ushirikiano mzuri na watu wa madhehebu na dini nyingine katika kuuendesha mradi huo ili uweze kuwa chachu ya maendeleo kwa maeneo mengine hasa vijijini ambako ndiko alizeti hulimwa.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment