Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

February 28, 2013

MWALIMU AFA KWA KUPIGWA RISASI NA POLISI ALIYEKUWA LINDO BANK YA NMB TAWI LA MAKETE KISA ELEMENT YA PIKIPIKI


 Mwili wa Mwalimu Casto Sote Kawamba aliyekuwa mwalimu wa shule ya Sekondari Kitulo aliepigwa risasi na askari wa jeshi la polisi wilayani Makete katika moka wa Njombe


             Tunaomba radhi kwa kuziweka picha hizo

Mwalimu mmjoa wa shule ya sekondari kitulo wilayani makete  aliyefahamika kwa jina la casto sote kawamba ameuawa kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la  polisi wilaya ya makete

Akizungumza na mtandao huuu ofisini kwake mkuu wa polisi wilaya ya makete SP Peter Kaiza kuhusu tukio hilo lililotokea eneo la benki ya nmb tawi la makete siku ya jana majira ya saa moja na robo asema kuwa mwalimu huyo alikuwa anakwenda kupata huduma za kibenk kupitia ATM akiwa na pikipiki ndipo alipo amuliwa na askari mmoja aitwae  Jose Msukuma  na kudai kuwa alikuwa hana herment alipoamuliwa kusimama alikaidi amri na kutaka kumgonga askari huyo aliye kuwa lindo 

Nae mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya makete Bw. Idd Nganya ambaye ndie mwajiri wa marehemu amesema kuwa mwili wa marehemu bado umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya makete  wakati  utaratibu wakuusafirisha mwili huo kwenda kwao mbeya kwa ajili ya mazishi ukiendelea

Nae mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye jina lake limehifadhiwa  amesema kuwa askari hao walikuwa wakiomba fedha kwa mwalimu huyo na baada ya kukatariwa ndipo walipo anza kumshushia kichapo na alipo wazidi walilazimka kutumia asilaha na kumpiga begani kwa upande wa mbele na ndipo mauti yalipomfika .


Kwa upande wao baadhi ya walimu wenzake na marehemu ambao walifika hospitali kujua kuhusina na kifo cha mwalimu mwenzao wameraani tukio hilo na kusema kuwa nilakikatili  na linapaswa kukemewa 

Aidha mganga mkuu mfawidhi ambaye ni msemaji wa hospitali ya wilaya ya makete Dkt.Michael gulaka amesema kuwa wao walipokea mwili wa marehemu nasio  majeruhi


Na Riziki Mgaya,Makete

No comments: