TAASISI ya kuzuia na
kupambana na rushwa katika Wilaya ya Ludewa Mkoa wa Njombe imehoji wadau zaidi
ya 60 wa elimu katika utafiti wake katika kubaini rushwa katika mimba kwa
wanafunzi wa sekondari.
Akitoa taarifa ya
utafiti katika warsha ya siku moja iliyofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya
wilaya hiyo mkuu wa taasisi hiyo wilaya Edings Mwakambonja alisema ofisi yake
iliamua kufanya utafiti huo kama njia ya kuwanusuru watoto wa kike ambao
wamekuwa wakitelekezwa baada ya kupata mimba kwa wazazi kunufaika kwa kulipana
na wahalifu.
Mwakamboja aliwaambia
washiriki wa warsha hiyo kuwa madhumuni ya utafiti wake ni kubaini mianya ya
rushwa katika kesi za mimba kwa wananfunzi wa sekondari katika halmashauri ya
wilaya ya Ludewa.
,,,, tunataka kubaini
pia mianya ya rushwa kwa watendaji wa vijiji, kata na walimu wakuu kujihusisha
na vitendo vya rushwa na kuwalinda watuhumiwa wanaohusika na kuwapa wanafunzi
mimba.,,,, alisema mwakambonja
Mwakambonja akaongeza
kuwa ofisi yake ilitaka kubaini pia endapo wazazi na wanafunzi wanaopata mimba
wanapokea hongo kutoka kwa watuhumiwa ili wasichukuliwe hatua za kisheria na
kubaini kama endapo sheria, kanuni na sera za elimu kama zinafuatwa ili
kuwawajibisha wahusika.
Aidha mwakambonja
alieleza eneo la utafiti na namna alivyopata sampuli kuwa ni pamoja na kuhoji
jumla ya watu 92 wakiwemo wanafunzi 40, wananchi 20, mkuu wa polisi wilaya ya
Ludewa (OCD) na afisa elimu sekondari.
Wengine ni waratibu
kata 9 maafisa watendaji kata 9 maafisa watendaji wa vijiji 12 na kwamba nia ya
kuwahoji wadau hao ni kupata taarifa za msingi na kuzingatia miongozo na sera mbalimbali
za elimu ili kukusanya na kuthibitisha uzingativu wa sera na miongozo hiyo.
MWAKAMBONJA matokeo
ya utafiti huu yanaonesha kwamba watuhumiwa wanaowapa wanafunzi mimba hutoa
hongo kwa watendaji na wazazi wa wanafunzi ili kukwepa vyombo vya dola kwa
kufanya usuluhishi.
Akitoa ufafanuzi
Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Ludewa Fredrick Lukuna kuna haja
ya kuwa na mashine za kupimia (DNA) kila wilaya ili kurahisisha na kubaini
ukweli mapema kuliko ilivyo sasa ambapo watu wamekuwa wakifuata huduma hiyo
jijini Dar es salaam ambako ni gharama.
Alisema ni kutokana
na kipimo hicho kuwa mbali ndiyo maana wazazi wamekuwa mstari wa mbele katika
kukubali kulipana kwa kigezo kuwa mtuhumiwa akifungwa atawaachia mzigo wa kulea
vijukuu.
,,, wakuu wa shule
wamekuwa wakitoa taarifa kwa watendaji kata lakini hawafanyi ufuatiliaji kuona
ni hatua zipi za kisheria zimechukuliwa kwa watuhumiwa waliohusika na uhalifu
wa kuwapa wanafunzi wao mimba.,,,, akalaumu Lukuna
Kaimu afisa elimu
sekondari Gelda Ng’asi akaongeza kuwa katika kuthibiti mimba na rushwa
mashuleni kuna haja ya wananchi/jamii na wazazi wenyewe kushirikiana na
kuunganisha nguvu zao na kuamua kukataa mimba za wanafunzi katika maeneo na
vijiji vyao.
Hata hivyo akaongeza
kuwa ili kuondoa tatizo la mimba mashuleni kuna haja ya wanafunzi wenyewe
kupewa elimu na kufanya kampeni ya kujitambua ili wajue athari za mimba shuleni
lakini pia sheria zirekebishwe kwa maana ya kutoa adhabu sawa kwa wavulana na
wasichana hiyo inaweza kujenga hofu.
Wilaya ya Ludea ina
jumla ya shule za sekondari 21 zikiwemo za bweni na kutwa na kati ya hizo shule
18 ni mali ya serikali na 3 zinamilikiwa na taasisi binafsi, wadau wa elimu
wamelalamkia shule hizo kuwa watuhumiwa wamekuwa hawachukuliwi hatua za
kisheria kutokana na kuendekeza rushwa.
mwisho
No comments:
Post a Comment