Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

February 16, 2013

MAMBA AUA MTU MTO LUHUHU, AMLA MWILI WOTE NA KUBAKIZA MIGUU.




           
MTU mmoja Ernest Fabiani Mahundi (56) mkazi wa kijiji cha Kiyogo Masasi Wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe ameua na mamba na kasha kumtafuna mwili wake na kubakiza miguu peke yake.

Kwa mujibu wa afisa mtendaji wa kijiji cha Kiyogo Samweli Gama  februari 10 mwaka huu marehemu Ernest Mahundi alivuka mto Luhuhu na kwenda katika kitongoji cha Lukali kilichopo kijiji cha Ngingama wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma kwa ajili ya kunywa pombe kama ilivyodesturi na alipokuwa akirudi akapatwa na mkasa huo.

Afisa mtendaji huyo akaongeza kuwa baada ya kugundua kupotea kwa marehemu aliitisha wananchi na kuanza kumsaka akiwa hai au amekufa na msako huo nulidumu kwa muda wa  siku mbili ambapo kiwiliwili cha marehemu kilipatikana maeneo ya kijiji cha ngelenge (fokland) kwenye kisiwa cha wavuvi akiwa ameliwa mwili wote na Mamba na kubakizwa miguu na kiuno huku kikiwa na suruali.
     

No comments: