Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

January 16, 2013

SHETANI USO KWA USO NA FILIKUNJOMBE




       
MZEE Leonadi Mhagama Shetani (115) mkazi wa kijiji cha Ludende Ludewa katika mkoa wa Njombe jana alitimiza ndoto yake ya kumwona mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe na kusema sasa mwenyezi mungu anaweza kumchukua katika dunia hii kwa sababu kiu yake ya kumwona mbunge imetimia.

Shetani ambaye ni muasisi wa chama cha mapinduzi(CCM)wilayani Ludewa amekuwa akikitumikia chama hicho kwa muda mrefu na kushiriki katika kampeni za chaguzi mbalimbali lakini kwa kuwa umri wake kuwa mkibwa amekuwa akishindwa kushiriki vikao vingi vya chama na kushindwa kuonana na mbunge wa jimbo la Ludewa.

Katika hali isiyo tarajia mzee Shetani aliwaambia wananchi waliokusanyika katika mkutano wa hadhara kuwa amekuwa akisononeka moyoni mwake kiasi cha kufa huku akimwomba mungu asimchukue kwanza mpaka atakapotimiza ndoto ya kuonana uso kwa uso na mbunge na kumshika mkono.

Alisema alikua na shauku ya kukutana uso kwa uso na mbunge huyo kijana kutokana na sifa anazozisikia katika vyombo vya habari namna mbunge huyo anavyokemea uovu kwa nguvu zote bila kuogopa vitisho vya wahujumu uchumi hao.

‘’’’’ nimekuwa nikiumia moyoni ni lini nitamwona mbunge huyu na wakati Fulani nikiugua nasononeka moyoni na kumuomba mungu asinichukue kwanza mpaka nipeane mkono na mbunge wangu kwa sasa hata mungu akinichukua sina kinyongo maana ndoto yangu imetimia.’’’’ Alisema kwa furaha mzee Shetani.

Filikunjombe alifika katika kijiji cha Ludende na kupokelewa kwa kuvalisha shada la maua na mzee shetani kama heshima ya mfalme kuwasili kijijini hapo kutokana na uchapakazi wake uliotukuka wa kuwatumikia wananchi.

Mzee Shetani alimsihi Filikunjombe kutokatishwa tamaa na watu wanaotaka kuliangamiza taofa kwa kutowatendea haki wananchi kwani yeye na wazee wengine wako nyuma yake kukemea tabia hizo.

Alisisitiza kuwa Tanzania ni nchi nzuri na inayoaminika na mataifa mengine kutokana na heshima ya muasisi wa nchi hii hayati Mwalimu Juliasi Kambarage Nyerere enzi za utawala wake.

Hivyo hangependa kuona chama alichokiacha muasisi wa taifa hili kinakuwa na viongozi wasio na uzalendo wan chi yao kwa kufanya ubadhirifu unsolididimiza taifa katika wimbi la umaskini badara ya kuwa na maendeleo tofauti na enzi zake.

Mzee Shetani alisema ni lazima kuwepo na viongozi wanaoweza kuthubutu katika kukemea uovu ndani ya chama na Serikali kama alivofanya hayati baba wa Taifa hili ili kuweka usawa wa kimaisha kwa watanzania.

Aidha Bw.Filikunjombe alisikiliza ushauri wa kada huyo na kuahidi kuutendea kazi kwa kutoteteleka katika maamuzi yake dhidi ya wanaoihujumu Serikali kwa kujilimbikizia mali za watanzania.

Filikunjombe alisema Tanzania inapaswa kuwa na watu wazalendo kama ilivyokuwa wakati wa uongozi wa hayati baba wa taifa na wazee wengine mfano wa mzee Shetani katika kutetea maslahi ya wananchi zaidi.

Alisema ni lazima viongozi wa sasa wawaenzi wazee hao wakati Taifa linapotaka maendeleo zaidi na kukabiliana na changamoto za kidunia zilizopo.

Mwisho.

No comments: