WANANCHI wa
tarafa ya Mwambao wa ziwa Nyasa wilaya ya Ludewa katika Mkoa wa Njombe
wameilalamikia idara ya elimu kwa kushindwa kusimamia na kukagua majengo yanayoendele kujengwa
chini ya kiwango na kuhatarisha usalama wa watotot wao imefahamika.
Wakizungumza
na gazeti hili kwa nyakati tofauti wananchi hao walisema walimu wakuu na kamati
za shule wamekuwa wakijenga madarasa na nyumba za walimu kwa ramani wanazozijua
wao kwa sababu wamekuwa wakifanya kazi za ukarandarasi na uhasibu wenyewe.
Hata hivyo
kutelekezwa kwa kitengo cha ukaguzi wa elimu nchini ndiko kumepoteza matumaini
ya ukuaji wa elimu kutokana na kitengo
hicho kutotazamwa kwa jicho la karibu ili kuinusuru elimu inayoporomoka kila
kukicha.
Hali hiyo imesababisha kushuka kwa kiwango cha ufaulu katika
shule za msingi na Sekondari nchini kukichangiwa na wizara ya Elimu kwa kiasi
kikubwa kutokana na kutotenga bajeti sahihi ya ofisi za ukaguzi hali ambayo
imesababisha walimu kutofanya kazi zao ipasavyo kutokana na kutokaguliwa.
Hayo yalisemwa jana na Kaimu afisa elimu ukaguzi wilaya ya
Ludewa Bw.John Haule alipotemblewa na gazeti hili ofisini kwake kuwa elimu ya
Tanzania inaelekea pahala pabaya kutokana na wakakuzi wa elimu kushindwa
kufanya kazi yao kwa kukosa fedha.
Bw.Haule alisema katika wilaya ya Ludewa kuna maeneo ambayo
ni zaidi ya miaka tisa sasa hayajakaguliwa mfano wa maeneo hayo ni kata za
mwambao wa ziwa nyasa,kata ya Lugarawa na kata za milimani hali ambayo
inazorotesha elimu nchini.
Alisema kitengo cha ukaguzi nchini kimetelekezwa kutokana na
kupangiwa bajeti hafifu ambayo haiwezi kukidhi haja kwa wafanyakazi wa kitengo
hicho kwani uendeshaji wa ofisi hizo umekuwa mgumu kutokana na kutokuwa na
stationary.
Akiitaja bajeti ya mwaka jana alisema kwa mwaka wa fedha 2011
hadi 2012 jumla ya shilingi laki sita ofisi yake ilitengewa akiwa shilingi laki
nne kwaajili ya matengenezo ya Gari na shilingi laki mbili ni kwaajili ya vifaa
vya ofisi hali ambayo inasikitisha kwani hata tairi za gari kwa fedha hiyo
haitoshi.
“Tunapangiwa bajeti bila ya kuangalia hali halisi ya
mazingira tuayofanyia kazi,kwa upande wa mwambao wa ziwa nyasa safari moja ya
ukaguzi inagharimu zaidi ya shilingi milioni moja kwa kua tunatumia usafiri wa
boti ambao hutumia lita 200 za petrol lakini fedha tunayopata inakatisha
tama”,alisema Bw.Haule.
Alisema walimu walio wengi katika maeneo yasiotembelewa na
wakaguzi hawatimizi wajibu zao hali ambayo huwafanya wafanye shughuri zao
binafsi na kuacha kuwafundisha wanafunzi kwa hali hii elimu nchini itazidi kudidimia.
Kwa upande wa waratibu Elimu kata kufanya ukaguzi Bw.Haule
alisema imekuwa ni vigumu kufanya ukaguzi kwani waratibu hawana bajeti kabisa
na hutengemea fedha kutoka kwa walimu wakuu ambazo huwasaidia kununulia
karatasi katika ofisi zao,hali ambayo huwashinda kuwakagua walimu wakuu.
Alisema kama waratibu elimu kata wangekuwa na bajeti yao
ingelikuwa ni rahisi kufanya kazi za ukaguzi na kuandika ripoti inayoonesha
mapungufu ya shule furani lakini hwawezi kumkagua mtu anaye wasaidia na
kumuandikia ripoti chafu.
Aidha aliitaja bajeti waliyotengewa idara ya ukaguzi wilaya
ya Ludewa kwa mwaka wa fedha 2012-2013 ni shilingi milioni moja fedha ambayo
bado wanaifuatilia hazina lakini haitoshi kwa lolote kwani maeneo ya mbali
haitakidhi pia gari ya ukaguzi haitaweza fanya safari kutokana na uchakavu wa
tairi zote.
Bw.Haule alitoa wito kwa Serikali kukihamisha kitengo hicho
kwenda TAMISEMI hali ambayo ingeweza kuboresha elimu nchini kutokana n kufanya
ukaguzi wa mara kwa mara ili kuweza kuwahimiza walimu kufanya kazi inayotakiwa
na wizara ya Elimu.
Mwisho
No comments:
Post a Comment