Mbunge wa jimbo la Ludewa Bw.Deo Filikunjombe amewahakikishia
wananchi wake kuwa na matumaini ya ujenzi wa chuo cha VETA kuanzia julai mwaka
huu katika kijiji cha shaurimoyo kata ya Lugarawa ili kwenda sambamba na migodi
inayotarajia kuanzishwa.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha
Shaurimoyo Filikunjombe alisema Serikali imeamua kufanya ujenzi huo kutokana na
umuhimu wa wilaya hiyo na migodi inayoendelea ili kupata wataalamu watakaofanya
kazi katika migodi hiyo.
Alisema ni fulsa pekee kwa wananchi wa wilaya ya Ludewa
kuchangamkia elimu itakayotolewa na chuo hicho ili kuweza kuajiliwa na
wawekezaji pia kujiajili katika mambo mbalimbali ndani na nje ya wilaya hiyo.
Bw.Filikunjombe alisema ujenzi wa chuo cha VETA wilaya ya
Ludewa umekuwa ukipigwa danadana kwa muda mrefu bila mafanikio lakini kwasasa
umefika wakati hata kama Serikali haina pesa za kutosha kujenga chuo hicho
wananchi wako tayari kujitolea nguvu zao ili chuo hicho Kijengwe.
“Mimi na wananchi wangu tuko tayari kujitolea nguvu zetu ili
chuo hiki kijengwe kwani ni ukombozi mkubwa kwa wilaya yangu kutokana na wilaya
hii kutokuwa na chuo cha ufundi tangia wilaya ianzishwe na tunaamini vijana wa
wilaya hii wanauwezo mkubwa kiakili katika kusoma fani mbalimbali
zitakozofundishwa hapa chuoni”,alisema Filikunjombe.
Alisema kutokana na uanzishwaji wa miradi mikubwa ya
uchimbaji wa chuma cha Liganga na Makaa yam awe ya Nchuchuma imepelekea chuo
hicho kujengwa kwa haraka ili wahitimu wa fani mbalimbali kuajiliwa katika migodi hiyo.
Aidha aliwataka wananchi wa wilaya ya Ludewa hususani kijiji
cha Shaurimoyo ambako ndiko chuo cha VETA kitajengwa kuwaandaa vijana wao ili
waweze kusoma katika chuo hicho kwani wasipo fanya hivyo watabaki kuwa
watazamaji kwa watu wengine watakaokuja kusoma.
Mkurugenzi mkuu wa VETA Tanzania Bw.Zebadia Moshi
aliwahakikishia wananchi hao kuwa Julai mwaka huu chuo hicho kitaanza ujenzi
rasmi na ifikapo Julai mwakani masomo yanatakiwa kuanza kutolewa rasmi ili
kwenda sambamba na uanzishaji wa migodi inayokuja.
Bw.Moshi alimsifu mbunge wa Ludewa Bw.Filikunjombe kwa
ufuatiliaji wake mpaka chuo hicho kujengwa wilayani Ludewa kwani chuo hicho
hakikupaswa kujengwa mwaka huu kutokana na ufinyu wa bajeti katika ofisi yake.
Alisema katika takwimu zake kwa mwaka 2013 ilitakiwa vijengwe
vyuo vine na si wilayani Ludewa lakini kutokana na umakini wa mbunge wa jimbo
hilo vimeongezwa vyuo viwili kikiwemo chuo cha Ludewa hivyo wananchi wanatakiwa
kumshukuru mbunge wao.
“katika ofisi yangu sikuwa na ratiba ya kujenga chuo mwaka
huu ndani ya wilaya ya Ludewa lakini kwa usumbufu wa Mbunge wenukwa waziri
anayesimamia wizara husika imebidi Ludewa ipate nafasi ya ujenzi wa chuo tena
haraka “,alisema Bw.Moshi.
Bw.Moshi aliwataka wananchi kujitolea nguvu zao ili chuo
hicho kijengwe kwa muda muafaka kwani kwa kufanya hivyo kinaweza kuleta manufaa
mapema zaidi kwa wananchi tofauti na watu wa maeneo mengine wanavyofikiri.
MWISHO
No comments:
Post a Comment