Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

October 15, 2012

OFISI YA MKUU WA WILAYA LUDEWA YATUNISHIANA MISURI NA TUME YA KATIBA


Na Nickson Mahundi,Njombe


MKUU  wa wilaya Ludewa  katika mkoa wa Njombe Juma Madaha ameitaka tume ya ukusanyaji wa maoni ya katiba  kutoa maelezo kwa maandishi kufuatia tume hiyo kushindwa kufika katika tarafa ya mwambao wa ziwa nyasa kukusanya maoni.

Akizungumza ofisini kwake jana Madaha alisema ratiba iliyopangwa ilizingatia taratibu zote za tume hiyo kufika katika kila tarafa lakini tume hiyo ilivunja ratiba kwa kufuta kata zote tano za tarafa yamwambao na badala yake ikaingiza kata mbili  za tarafa ya Liganga.

Bw.Madaha ameonesha masikitiko yake kutokana na tume hiyo kutokufika tarafa ya mwambao kwa madai kuwa kuwa hali ya miundombinu ya barabara kuwa mibaya jambo ambalo siyo kweli.

“” mbona mimi pamoja na viongozi wengine tumekuwa tukifanya ziara katika maeneo hayo bila wasiwasi hizo taarifa za barabara kuwa mbovu wamezipata wapi hakuna sababu ya kutokwenda huko kwa sababu wananchi wanahaki ya kutoa maoni kama watanzania wengine.” Alisisitiza Madaha

Alisema hali hiyo haiwezi kufumbiwa macho kinachotakiwa tume itoe maelezo yatakayowafanya wananchi wa mwambao mwa Ziwa Nyasa kuielewa na kuiamini Serikali yao kwani wamekuwa wakipuuzwa kwa mambo mengi ikiwemo kutotembelewa na viongozi wa Mkoa na kitaifa.

Wananchi wa kata za Kolondo, Makonde, Lumbila, Lifuma wakaenda mbali zaidi na kusema kuwa wamekuwa wakichangishwa fedha za mwenge lakini mwenge wenyewe hawaujui kwa kuwa haujawahi kufika katika maeneo yao.

Hata hivyo kuna taarifa za kutatanisha  kutoka kwenye mjumbe mmoja ndani ya tume hiyo aliyetaka jina lake lisiandikwe gazetini aliliambia gazeti hili kuwa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ludewa ndiyo iliyohusika na kuvunja ratiba hiyo baada ya ofisa wake aliyetajwa kwa jina la Charles Keiya ambaye ni afisa tawala kutoa vitisho kwa tume hiyo kuwa barabara ni mbovu haipitiki kirahisi.

Akitoa maelezo kuhusu tume kukatisha ziara tarafa ya mwambao
Bw.Charles Keiya ambaye alilalamikiwa kuhusika moja kwa moja kuibadiri ratiba kutokana na yeye kuwa katika msafara wa ukusanyaji wa maoni ya katiba mpya alikana kuhusika na hilo na kusema huo ulikuwa ni uvumi wa wananchi.

Aidha Bw.Keiya alishindwa kuthibitisha kwa mkuu wa wilaya kuhusu kauli aliyotoa kuwa tume ilitishwa na wananchi wa Ludewa kuhusiana na barabara za kata za mwambao jambo lililopelekea tume kushindwa kufika mwambao wa ziwa nyasa na kuzua malalamiko ikiwa ni pamoja na serikali kuwatenga wananchi hao kwa mambo mengi.

“wananchi waliwatisha viongozi wa tume kuwa barabara za Mwambao mwa ziwa Nyasa ni mbaya na hazipitiki,hivyo nikawa sina namna ila nimewashauri wawalete vijana ambao wataweza kwenda huko kwani waliokuja ni wazee na hawawezi misukosuko”,alisema Bw.Keiya.

Aidha Bw.Keiya amekuwa akilalamikiwa kwa mambo mengi na wa
Fanyakazi Halmashauri ya wilaya ya Ludewa hususani katika misafara mbalimbali ya wageni wa kitaifa kwa kutengua mambo  yanayopangwa katika vikao vya pamoja na kujiamulia mambo yake binafsi.

Hata hivyo wananchi wa kata za mwambao wameulalamikia uongozi wa wilaya ya Ludewa kwa kutengua ratiba iliyopangwa awali na kuendelea kuwadanganya na kusababisha kukosa  haki yao ya msingi katika kutoa maoni ya uundwaji wa katiba ya nchi yao kama watanzania.

Mwisho.

1 comment:

Anonymous said...

That's really interesting. Thanks for posting all the great information! Had never thought of it all that way before.