Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

October 14, 2012

MWENYEKITI WA MARADI WA CHAMPION NA MUASISI WA NURU FM BW MLONGWA MKUCHU AFARIKI DUNIA


Mwnyekiti wa mradi wa champion mkoa wa Iringa Bw.Mlongwa Rojas Mkuchu amefariki Dunia leo asubuhi katika hospitari ya Ocen Road jijini Dar es salaam alikokuwa akitibiwa

Meneja  wa  kituo cha radio Nuru Fm Bw.Victor Chakudika ameuarifu mtandao  huu  wa www.habariludewa.blogsport.com   kuwa aliyepata kuwa mwandishi wa shirika la IDYDC katika ukusanyaji wa habari za vijana ,shirika ambalo linamiliki kituo hicho cha Radio Nuru Fm Mlongwa Mkuchu amefariki dunia leo asubuhi katika Hospitali ya Ocen Road jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akitibiwa .

Bw.Mlongwa aliwahi kufanya kazi pia kwa karibu kama mratibu wa ukimwi katika shirika la IDYDC na hayati.Philoteus Njuyuwi kuanzia mwaka 2004 hadi mwaka 2007 ndipo aliachana na kazi hiyo na kuingia katika miradi mingine mkoani iringa.

Atakumbukwa kwa mengi kutokana na utendaji wake wakazi kutokana na kuweza kuzitembelea wilaya zote za mkoa wa Iringa ikiwemo wilaya ya Ludewa kutokana na elimu yake kama muwezeshaji wa mafunzo mbalimbali katika jamii.


Taarifa zinaeleza kuwa alikuwa akisumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa kansa katika mgongo wake kwa miaka miwili na kupelekwa katika Hospitali hiyo.

Mbali ya mchango wa Mlongwa  kuwa mkubwa katika jamii enzi za uhai  wake bado Mlongwa atakumbukwa kwa mambo mbali mbali ya kijamii ambayo amepata  kuyafanya enzi  za uhai wake katika kuielimisha jamii ya mkoa  wa Iringa juu ya janga la UKIMWI kupitia mradi wa WANAUME TUWAJIBIKE .


Kwa wadau  wa mtandao huo msiba wa Mlongwa  pia ni pigo kubwa  kutokana na mchango mkubwa ambao mke wake Jamida Kulangwa ambao aliutoa kwa mtoto Juliana Mwinuka wa kijiji cha Mavanga Ludewa ambaye aliungua kwa moto na kuendelea  kutaabika nyumbani kwa zaidi ya miezi sita bila kusaidia hadi mwanamke  huyo Jemida alipofikisha taarifa zake katika mtandao huu na kuanza kusaidia kabla ya kwenda kijijini kumfuata mtoto  huyo kwa kushirikiana na msamaria mwema mmoja mkazi wa jiji la Dar es Salaam na mkazi wa Ludewa  walikubali kujitolea kuacha shughuli zao na kwenda kumchukua mtoto huyo .


Hadi leo Jemeda anapatwa na tatizo  hilo ndie alikuwa msaada mkubwa wa  kumuuguza mtoto huyo akishirikiana na mdau  huyo mkazi wa jiji la Dar es Salaam na Jemida  alikuwa akimuuguza mtoto Juliana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili aliko sasa  huku akiendelea  pia kumuuguza mume  wake katika Hospitali ya Ocen Road hadi kifo kinapomkuta.


Mtandao  huu unaendelea kumpa moyo mdau Jemida Kulangwa  kupiga moyo konde katika kipindi hiki kizito kwake na kuwaomba  wadau  kuendelea  kumsaidia mtoto Juliana Mwinuka pia.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE

No comments: