Na Nickson Mahundi,Njombe.
Sekta ya utalii katika mkoa
wa Njombe imeelezwa kusahaulika katika mkoa w licha kuliingizia taifa
kipato kutokana na wageni mbalimbali wanaotembelea vivutio hivyo kwa ajili ya
kujionea maajabu mbalimbali.
Licha ya mkoa wa Njombe kuwa
na vivutio vingi vya utalii, ikiwamo hifadhi ya wanyama ya kitulo, shamba la maua yenye kuvutia na kustaajabisha
lilopo Uwemba na mwamba wenye ramani ya afrika unaopatikana
katika Kijiji cha Igodiva Tarafa ya Imalinyi wilayani Wanging’ombe lakini hakuna kinachoendela.
Hata hivyo kutokuwapo kwa
juhudi za kutosha katika kuhamasisha
wananchi kutembelea vivutio
hivyo kumechangia vivutio vingi vya utalii kutofahamika hata kwa baadhi ya
wenyeji wa mkoa wa Njombe, kwani wakazi wengi wa mkoa huo bado wanaamini
kwamba sekta ya utalii hapa nchini ipo katika mikoa ya kusini pekee.
Akizungumza na gazeti hili
afisa utalii, mali asili na mali kale wa
wilaya ya Njombe Bw.Abed
Chaula alikiri kuwa wakazi wa mkoa huu
kutokuwa na mwamko wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo hapa hali
ambayo inachangia kutofahamika kwa vivutio hivyo kwa baadhi ya wakazi mkoa wa
Njombe.
“Baadhi ya wakazi wengi wa
mkoa huu hawana mwamko wa kutembelea vivutio vya utalii kwa kuzani kuwa
anayepaswa kutembelea vivutio hivyo ni watalii kutoka nje ya nchi pekee, lakini
wengine wako hapa mkoani hawajui vivutio vya utalii vilivyopo mkoani hapa
wakiamini kuwa fursa ya utalii ipo katika mikoa ya kusini pekee,” alisema
Chaula.
Sanajari na hayo alikiri
kutofanya jitihada za makusudi katika
kuvitangaza vivutio vya
utalii vilivyopo mkoani hapa pamoja na kutoa hamasa ya kutosha kwa wananchi
hususani wenyeji wa mkoa wa Njombe kutembelea vivutio hivyo vya utalii.
Hata hivyo alitoa wito kwa
wananchi wa Njombe kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii ili kuwa
mabolozi wazuri wa vivutio hivyo.
“Nawaomba wakazi wa Njombe
kuwa na utaratibu wa kutembelea vituo vya utalii, unajua ni aibu mgeni anakuja
anakuuliza kivutio cha utalii kilichpo katika eneo lako halafu mwenyeji
hukijui,’’ alisema Bw.Chaula.
Aidha Chaula alisema kukua
kwa sekta ya utalii katika mkoa kutasaidia kupatikana kwa fursa nyingi za ajira
na hivyo kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira nchini.
Vingine ni safu ya milima ya Livingstone,misitu ya miyombo na fukwe za ziwa Nyasa vyote hivyo vinapatikana katika wilaya ya Ludewa katika mkoa huu wa Njombe.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment