Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

September 15, 2012

MSANII WA NYIMBO ZA INJILI AVUNA PESA WILAYANI LUDEWA

Na Nickson Mahundi

Msanii wa nyimbo za injili wilayani Ludewa Bi.Anterma Luoga mwishoni mwa wiki iliyopita alijipatia zaidi ya milioni sita katika tamasha la uzinduzi wa video yake inayotambulika kwa jina la Tumekombolewa kwa Neema.
Bi.Anterma Luoga akiwa katika kanisa la E.A.G.T wilayani Ludewa.

Katika tamasha hilo wasanii wengi wanaochipukia katika tasnia ya muziki wa Injili waliweza kuonesha vipaji vyao na kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki huo ambapo ilifanyika harambee ya michango ya fedha ili kuweza kuwasaidia wasanii hao  kurekodi nyimbo zao kama alivyofanya mwenzao.

Aidha tamasha hilo lililohudhuriwa na watu maarufu wilayani kama mzee Mwasanga,Diwani wa kata ya Ludewa Bi.Monika Mchilo na Mbunge wa jimbo la Ludewa Bw.Deo Filikunjombe ambaye alikuwa mgeni rasmi wa tamasha hilo.

Bw.Filikunjombe alitoa shilingi milioni mbili kwa msanii huyo na kuahidi kuendelea kumsaidia ili aweze kutimiza ndoto zake katika tasnia hii ya muziki wa Injili ambao unapendwa na watanzania wengi katika kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa jamii.

"Napenda kuwakumbusha waimbaji wote wenye vipaji vya kuimba endeleeni na mwendo huo kwani unaweza jipatia kipato kwa kazi hii,ila kumbukeni kuwa sio wote wanaopenda maendeleo ya mtu,mtapambana na vikwazo vingi lakini kama mtamtanguliza Mungu mtashinda majaribu hayo", alisema Filikunjombe.

Katika hatua nyingine Bw.Filikunjombe alitoa ahadi ya kumsaidia Bi.Rose Msigwa kurekodi nyimbo zake kuanzia audio na video kutokana na Binti huyo kuonyesha kipaji cha hari ya juu lakini amekuwa akishindwa kurekodi kutokana na kukosa fedha ya kufanyia kazi.

Hata hivyo Askofu Mlowe alimaalufu kwa jina la Ngapunda wa kanisa la E.A.G.T  aliwashukuru wageni waliohudhuria katika tamasha hilo na kuwataka kuwasaidia wasaii hao kwa ugumu wa kipato ndicho chanzo cha kukwama katika juhudi zao za kujikwamua kiuchumi na kulitangaza neno la Mungu kwa njia ya nyimbo.


Enhanced by Zemanta

1 comment:

Anonymous said...

Gud start