Mkuu wa
wilaya ya Ludewa Mh.Andrea Tsere ameipongeaza mitandao ya kijamii wilayani hapa
kutokana na mitandao hiyo kuchangia kiasi kikubwa katika mendeleo ya wilaya katika
maafa pia elimu.
Pongezi hizo
zimekuja baada ya kikundi cha mtandao kwa njia ya whatsup kijulikanacho kwa
jina la group la wilaya ya Ludewa kuandaa mpango wa wanafunzi wa vyuo vikuu
wanaotokea wilaya ya Ludewa kujitolea
kufundisha shule za sekondari msimu wa likizo.
Mpango huo
unakwenda sambamba na uchangishaji wa fedha katika group la wilaya ya
Ludewa,fedha ambazo zitatumika kujikimu kwa wanavyuo ambao wataonesha nia ya
kwenda kuinua kiwango cha ufaulu katika shule za Sekondari ndani ya wilaya ya Ludewa.
Mh.Tsere
alisema kuwa mpango huo ni wakuigwa kwani mitandao mingi ya kijamii imekuwa
ikitumika katika siasa na mambo mengine ya hovyo badala ya kujikita katika
kuleta maendeleo kwa wananchi kama inavyofanywa na group la wilaya ya Ludewa.
“niwapongeze
kwa juhudi za group hili la wilaya ya Ludewa kwa kuandaa mpango wa maendeleo na
kuchangishana fedha ili kuwapatia posho wale watakao jitolea kwani si mara ya
kwanza katika group hili kuchangia maendeleo,wamesha saidia ununuzi wa kitanda
cha wagonjwa hospitari ya wilaya pia walichangia wakati bweni la shule ya
sekondari chief Kidulile lilipoungua hivyo ni mfano wa kuigwa”,alisema
Mh.Tsere.
Aidha
Mh.Tsere aliwataka wananchi wilayani Ludewa kutoa ushirikiano kwa walimu
wanaokuja kujitolea kwani hawalipwi na Serikali hivyo kila mwananchi anawajibu
wa kuwalinda kwani wilaya ya Ludewa inaupungufu mkubwa wa walimu wa masomo ya
Sayansi hivyo ni fulsa pekee kuwatumia walimu hawa wakujitole ili kukuza
kiwango cha ufaulu.
Akitoa
ufafanuzi wa mgawanyo wa walimu hao katika shule za Sekondari afisa elimu wa
wilaya ya Ludewa shule za Sekondari Mwalimu Matenus Ndumbalo alisema kuwa
tayari amewasiliana na walimu wakuu wa shule za Sekondari zote wilayani hapa
ili kuwapokea walimu hao.
Mwalimu
Ndumbalo alisema kuwa ni kweli wilaya ya Ludewa kunaupungufu mkubwa wa walimu
wa masomo ya Sayansi hivyo ni fulsa pekee katika mpango huu wa walimu wa
kujitolea ili kuongeza ufanisi katika elimu kwani mpango huu ungeanza muda
mrefu ni dhahiri wilaya ya Ludewa ingepiga hatua kielimu.
Mwalimu
Ndumbalo aliwataka wanagroup la wilaya ya Ludewa muufanya mpango huo kuwa
endelevu kila mwaka ili ufaulu hasa katika masomo ya Sayansi kuongezeka na
kushindanda na wilaya nyingine nchini.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment