Mkurugenzi wa Nicopolis Augustino Mwinuka akikabidhi mchele
Mratibu elimu kata ya Ludewa Mwalimu Lenis Mtitu
Makamu Mwalimu mkuu shule ya msingi Kimbila Imani Mtweve akiongea na wageni kutoka Nicopolis Academy na Ludewa education Centre
Baadhi ya majengo ya shule ya msingi Ludewa Mjini
Mkurugenzi wa Nicopolis Academy Mwalimu Augustino Mwinuka akiongea na wanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Ludewa mjini mara baada ya kukabidhi msaada wa mchele
Mkurugenzi wa Nicopolis Academy Mwalimu Augustino Mwinuka akiongea na wanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Ludewa mjini mara baada ya kukabidhi msaada wa mchele
Kulia Mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Ludewa mjini Mathew Haule akiwa na wageni wa Nicopolis pamoja na Ludewa Education
Wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Kimbila wilayani Ludewa wakiwa darasani
Kituo cha
watoto waishio katika mazingira hatarishi wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe
cha Nicopolis academy pre &primary English medium school kwa kushirikiana
na Ludewa education Centre wametoa msaada wa chakula kwa wanafunzi wa darasa la
saba katika kata ya Ludewa.
Akikabidhi
msaada huo kwa walimu wa shule za msingi kata ya Ludewa mkurugenzi wa Nicopolis
Academy Mwalimu Augustino Mwinuka alisema kuwa wamefikia hatua ya kutoa msaada
huo wa mchele kwa wanafunzi wa darasa la saba ili kuwawezesha kupata chakula
siku mbili za mtihani wa Taifa unaotarajia kufanyika hivi karibuni.
Mwalimu
Mwinuka alisema kuwa baadhi ya wazazi na jamii kwa ujumla wamekuwa wakutoa
lawama kwa walimu pale matokeo yanapokuwa mabaya bila kujali wao kama jamii
wanamchango gani kwa wanafunzi hasa kipindi cha mitihani ya mwisho,hivyo kabla ya
kulaumu ni vyema kutambua wajibu wa jamii kwanza ndipo zitolewe lawama kwa
walimu.
Alisema kuwa
watoto wanapopata chakula cha aina moja kipindi cha mitihani inaweza kusaidia katika
ufaulu kwani ikiwa kila mmoja atapata chakula kutoka nyumbani kwake wengine
hawana uwezo mzuri wanakotoka hivyo hujikuta wanyonge wanapoona wenzao
wanaletewa vyakula vya aina Fulani na wazazi wao na hali hiyo hupelekea kufanya
vibaya katika chumba cha mtihani.
“sisi kama
Nicopolis academy na Ludewa education centre tumeona tutoe mchele huu kidogo
kwa shule za kata ya Ludewa,tunaomba na wadau wengine watuunge mkono kwani
uwezo wa wazazi umetofautiana,mwingine anamuahidi mtoto wake atamletea chipsi
hivyo mtoto akiwa darasani atashindwa kufanya mtihani akibaki na mawazo kuwa
leo lazima niwaoneshee wezangu kwa kula chipsi hivyo kwa chakula cha pamoja
haitatokea hilo,”alisema Mwalimu Mwinuka.
Alisema kuwa
Nicopoli Academy inawafadhiri hivyo ikaona ufadhiri huo ni vyema shule nyingine
zikanufaika kwani Mwalimu Mwinuka aliahidi kutoa usafiri kwa wanafunzi wa shule
ya msingi Songambele waishio Ngalawale kwa kipindi hiki cha mtihani kwani
wamekuwa wakitembea umbali mrefu unaokadiriwa kilometa 6 hadi shuleni hapo.
Aidha
akishukuru kwa msaada huo mratibu wa Elimu kata ya Ludewa Mwalimu Lenis Mtitu alivipongeza
vituo hivyo kwa kuona umuhimu wa kuwasaidia chakula wanafunzi wa darasa la saba
hasa kipindi cha mitihani kwani ni ukweli usiopingika uwezo wa kifamilia
haulingani hivyo wata wazazi wanapowaletea watoto wao chakula kipindi hiki
lazima utofauti utatokea.
Mwalimu
Mtitu alisema kuwa kama jamii na wadau mbalimbali wataelimishwa nini wanatakiwa
kukifanya kwa watoto wao kipindi cha mitiahani basi hata ufaulu unaweza
kuongezeka kutokana na hali halisi za kifamilia kwa kuna wanafunzi wengine
hushindwa kurudi majumbani mwao mchana kupata chakula huvyo hulazimika kukaa na
njaa wakisybiri mtiahani.
Hata hivyo
Mratibu elimu kata huyo alivitaka vituo hivyo kuendeleza tabia hiyo na kuwataka
wadau wengine wa elimu kuiga mfano huo ambao unaleta tija katika sekta ya elimu
ikiwa pamoja na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment