Mh.Andrea Tsere akimkabidhi Jezi Kocha wa Mapinduzi Quens Fc Bw.Hilaly Lugome
Matha Luoga akikabidhiwa jezi na mkuu wa wilaya ya Ludewa Mh.Andrea Tsere
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Mh.Tsere akiongea na wananchi pembeni yake ni mshauri wa mgambo wa wilaya ya Ludewa
Mh.Andrea Tsere akimkabidhi Jezi Matron wa Mapinduzi Quens fc Bi.Evelina Mgaya
Bi.Zaina Mlawa katibu tawala wa wilaya ya Ludewa akikadhi jezi tayari kwaajili ya kuukabidhi uongozi wa Mpinduzi Quens Fc
Mkuu wa wilaya ya Ludewa Mh.Tsere akiongea na wananchi
Evelina Mgaya akiwa pamoja na baadhi ya wachezaji
Mh.Tsere akiongea na baadhi ya vijana wanaopata mafunzo ya Mgambo
Mh.Tsere akiongea na baadhi ya vijana wanaopata mafunzo ya Mgambo
Mh.Tsere akiongea na baadhi ya vijana wanaopata mafunzo ya Mgambo
Mkuu wa
wilaya ya Ludewa katika mkoa wa Njombe Mh.Andrea Tsere ameikabidhi rasmi timu
ya mpira wa miguu wasichana ya wilayani Ludewa ya Mapinduzi Quens fc jezi
ambazo waliziomba kwa Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Mh.Majaliwa Kassim Majaliwa wakati wa
ziara yake iliyafanyika wilayani hapa.
Akikabidhi
jezi hizo jana katika uwanja wa mpira wa miguu wa Halmashauri ya wilaya ya
Ludewa Mh.Tsere alisema kuwa Waziri mkuu ni mdau wa michezo na anatambua umuhimu
wa michezo hivyo ametimiza ahadi yake aliyoihaidi kwa timu hiyo hivyo kwa
kuonesha umuhimu wa mchango wake katika timu ya mpira wa miguu wasichana wilaya
ya Ludewa ni vyema kuiendeleza timu hiyo ili ifanye vizuri katika mashindano ya
mkoa na Taifa.
Alisema kuwa
Mh.Mjaliwa ameanza kuwa kuisaidia Jezi lakini wadau mbalimbali ikiwa pamoja na
wanaludewa wanatakiwa kuisaidia timu hiyo kwani bado inaupungufu mkubwa wa
vifaa vya michezo hivyo kama yeye mkuu wa wilaya aliahidi kuichangia Mapinduzi
quens mipira miwili ili iendelee na mazoezi ya kila siku.
“Mh.Majaliwa
ametuunga mkono kwa kutupatia Jezi lakini sisi kama wanaludewa tunatakiwa
kuhakikisha timu yetu inasonga mbele kwani wilaya yetu inavipaji vya kutosha
hivyo haina sababu ya kuvipoteza vipaji hivi zaidi ya kuviendeleza
kinachotakiwa ni kuungana na mwalimu wa timu hii pamoja na uongozi wao
kuifikisha pahala”,alisema Tsere.
Awali akitoa
shukrani kwa Waziri mkuu kwa kutoa msaada wa jezi hizo mwalimu wa Timu hiyo
Bw.Hilaly Lugome alisema kuwa timu hiyo ambayo imepata sale kutoka kwa
Mh.Majaliwa bado inachangamoto nyinge katika msimu huu ambao inatakiwa
kushiriki ligi ya mkoa.
Bw.Lugome
alimshukuru waziri mkuu kwa kuijali michezo na kwa kukamilisha ahadi yake
ambayo aliahidi katika mkutano wa hadhara hivyo bado wadau wanatakiwa kumuunga
mkono waziri mkuu kwa kuisaidia timu hiyo katika vifaa vingine vya michezo
ikiwa pamoja na viatu mipira na chakula kwaajili ya kambi.
Tukio hilo
la ugawaji wa jezi lilifanyika sambamba na ufunguzi wa mafunzo ya jeshi la
akiba la mgambo kwa kata ya Ludewa ambapo jumla ya vijana 42 wamejitolea kwa
hiyari yao kupata mafunzo hayo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment