Mh.Sendeka akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi
Ngoma ya Asili ya Mganda kutoka kata ya Lupingu ikitumbuiza katika sherehe za wafanyakazi
Mh.Sendeka akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi
Mh.Sendeka na viongozi wa vyama vya wafanyakazi wakiwa pamoja na waandishi wa habari
Mh.Sendeka akipata maelekezo kutoka kwa meneja wa kituo cha radio cha Best fm Bwana Godluck Mshairi kilichopo wilaya ya Ludewa katika mabanda ya maonesho ya Meimosi wilayani Ludewa
Idara ya maendeleo ya jamii wakitoa maelekezo kwa Mh.Sendeka
Tazara imemuomba Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuri kuzuia ubebwaji wa mizigo mizito
unaofanywa na magari ya mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam kuelekea nchini
Zambia kunafanya Treni za mizigo za reli hiyo kukosa mizigo na pia magari hayo
yanachangia uharibufu wa miundombinu ya barabara hali inayoitia hasara Serikali
ya Tanzania.
Kauli hiyo imetolewa jana na Mwalimu Fratern
Kwahhison katibu wa kamati ya meimosi na katibu wa CWT Mkoa wa Njombe kwa Mgeni
rasmi wa Serehe za Mei mosi mkoa wa njombe ambaye ni mkuu wa mkoa huo Mh.Christopher
Ole Sendeka sherehe ambayo kimkoa ilifanyika wilaya ya Ludewa na kudhuriwa na
viongozi mbalimbali kutoka katika wilaya za mkoa wa Njombe pia wananchi wa
wilaya ya Ludewa.
Akisoma risala hiyo Mwalimu Kwahhison alisema
kuwa sheria iliyopo inayosimamia taasisi ya Tazara inayoitwa Tazara ACT,haiendani
na hali halisi,serikali ya Tanzania na ile ya Zambia iangalie upya sheria hii
ili ilete tija kwani Tazara imekuwa ikishindwa kufanya biashara hasa katika
mizigo kutokana na mizigo mingi mikubwa kubebwa na magari hali inayoifanya
Tazara kushindwa kujiendesha.
Alisema kubwa magari hayo makubwa ya mizigo
yamekuwa ndio chanzo cha uharibifu wa barabara kutokana na uzito mkubwa na
kuitia hasara Serikali ya Tanzania kuwa na bajeti ya matengenezo ya barabara
kila mwaka hivyo ni vyema mizigo hiyo inngesafirishwa kwa kutumia reli ya
Tazara ili kuinusuru miundombinu ya barabara.
Katika risala hiyo pia Mwalimu Kwahhison aliitaka
Serikali kuangalia malimbikizo ya walimu
na kuyalipa kwa wakati ikiwa pamoja na upandishwaji wa madaraja kwani kimekuwa
kilio cha muda mrefu kisichotekelezeka ikiwa na upungufu mkubwa wa wafanyakazi
wa sekta ya Afya hasa vijijini,kushushwa vyeo vya ngazi ya mishahara kwa
maafisa Tarafa kutoka TGS F 5 hadi TGS 0 badala ya kubaki TGS 5 na kutolipwa
malimbikizo ya mishahara yao toka 2012 hadi sasa.
Alisema kuwa Mkoa wa Njombe ni miongoni mwa
mikoa isiyo na Mahakama ya Rufaa na ni mikoa ambayo inakua kwa kasi kwa kuwa na
raslimali nyingi zinazovutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi,hali hii
inasababisha matukio mengi ya kiuharifu kuongezeka kutokana na mwingiliano
mkubwa wa watu hivyo Serikali inaomba kulitatua tatizo hilo mapema.
Akitoa Hotuba katika sherehe hizo mkuu wa
mkoa wa Njombe Mh.Christopher Ole Sendeka ambaye ndio Mgeni Rasmi alisema kuwa
Serikali ya awamu ya tano iko makini kuhakikisha maslahi ya wafanyakazi
yanaboreshwa hivyo baadha ya zoezi la kuwatambua watumishi hewa neema inakuja
kwa wafanyakazi waadirifu na wachapakazi.
Mh.Sendeka alisema kuwa kuhusuana na suala
la Tazara litapatiwa ufumbuzi hivyo malalamiko hayo tayari Mh.Rais anayo,pia
kuhusiana na mkoa wa Njombe kukosekana kwa Mahakama ya Rufaa ni kweli jambo
hilo bado mkoa wa Njombe unatumia Mahakama ya Iringa kutokana na ukweli kwamba
mkoa wa Njombe ulitokana na Mkoa wa Iringa hivyo taratibu zinaendelea kufanyika
kujiondoa taratibu ktk mkoa Mama.
Alisema kuwa mamlaka nyingi zilikuwa bado
Iringa lakini taratibu Serikali imezihamisha na kuwa Njombe kama mkoa hivyo
hata hili la Mahakama ya Rufaa itafanyiwa kazi,pia aliwataka wafanyakazi
kutokuwa wanyonge kwani ofisi yake iko wazi muda wote na kama kuna kero
inayohusu wafanyakazi basi vyama vya wafanyakazi visisite kumuona ili kutatua
kero hizo.
Mwisho.
KWA UDHAMINI WA MTANZANIA RESTAURANT, WANAPATIKANA LUDEWA MJINI KATIKA JENGO LA NDICHELIWE.
KWA CHAKULA SAFI NA BORA UKIFIKA LUDEWA MJINI MTANZANIA RESTAURANT NDIO SURUHISHO PIA KWA CHAKULA CHA MAHARUSI,MISIBA MAHAFARI NA SHEREHE MBALIMBALI
KWA MAWASILIANO PIGA NO.0758146258 au 0624985168 KWA CHAKULA CHA UHAKIKA.
No comments:
Post a Comment